ZIFAHAMU FURSA ZINAZOLETWA NA TEKNOHAMA KATIKA MASUALA YA AJIRA


Katika makala hii tuangalie fursa zinazoletwa na teknohama katika maswala ya ajira. Fursa hizi nimezigawa katika makundi ya kutafuta kazi na  utendaji makazini.

1. Kutafuta Kazi :
Kupata ujuzi na uzoefu:
Kuandika CV:  Ukiacha fursa za kujisomea namna bora ya kuandika CV au barua za maombi ya kazi kama makala hii ya Mbuke Times (BOFYA HAPA), teknohama inakupa fursa ya kupata huduma za kukuongeza kubuni na kuandika CV yako vema. Huduma kama
Maombi ya nafasi ya kazi : Ukiacha websites kibao zinaweka matangazo ya nafas iza kazi, sasa kupitia Android na iphone apps unaweza kupata matangazo ya nafasi za kazi kibao. Cheki mfano Android app za indeed.com na Monster Job Search kwa simu yako ya Android.
Pia unaweza tumia website kama vile LinkedIn kujenga mtandao wa watu wanaoweza kukusaidia taaria za nafasi za kazi na pia kuitumia LinkedIn kujielezea na kuomba kazi.
Pia usisahau kuna makampuni na asasi kadhaa zilizojiwekea utaratibu ambapo unaweza jiandikisha moja kwa moja kuomba kazi kupitia websites zao.  Si rahisi kuweka orodha kwa sasa, ila nikutajie makampuni kama Vodacom na MTN hufanya hivyo.

Utendaji makazini

Mawasiliano : 
Team chats mfano wa Slack, na namna ya kupangilia taarifa za miradi na kuwasiliana kupitia Trello. 
Hivi karibuni Facebook imetangaza kutoa huduma maalum ya Facebook at Work, ambapo kampuni hiyo imetengeneza mtandaoni wa kijamii kama Facebook ila maalum kwa ajili ya wafanyakazi wa makampuni na asasi mbalimbali.
Ufanyaji kazi pamoja: Kupitia kurahisisha mawasiliano kwa video conferencing, kupitia program zinazoruhusu kuhifadhi hewani na kushare mafaili ya kazi. Huduma kama Google Docs ni mfano mzuri katika hili.

Uboreshaji wa mchakato wa ufanyaji kazi: 
Hata michakato cha uzalishaji na ufanyaji kazi kwa ujumla vinaboreshwa  kupitia teknohama. Virtual Reality Site inataja matumizi ya teknolojia ya virtual reality katika jeshi la marekani ambapo wanajeshi hupatiwa mafunzo ya jinsi ya kupambana na maadui kwa kutumia ulimwengu wa kutengenezwa unaofanana kabisa na hali halisi ya mahali watakapoenda kupambana.
Technrepublic.com inataja matumizi makubwa ya teknolojia ya virtual reality katika sekta ya matibabu kuanzia kwenye kusaidia wagonjwa kupata matibabu kwa haraka, na hata kwa madaktari kutumia teknolojia hiyo kuboresha uelewa wao wa matatizo yanayowakumba wagonjwa na mbinu za matibabu bora.

Kupunguza gharama za uzalishaji: 
Teknohama inapunguza gharama za mawasiliano na uendeshaji wa ofisi. Badala ya kuingia gharama kubwa za mawasiliano ya simu , baadhi ya waajiri hutumia huduma za kuchat , na kupiga simu kupitia mtandaoni kama vile Skype. Na waajiri wengine badala ya kuingia gharama ya kuwa na ofisi nyingi kwa ajili ya wafanyakazi wake, huruhusu wafanyakazi kufanya kazi sehemu yoyote ile nje ya ofisi ila mawasiliano na ofisi na usimamizi wa kazi unafanyika kupitia teknohama.
Na kuna baadhi ya waajiri hupunguza gharama za kusaili waombaji wengi wa kazi kwa kutumia huduma za usajili mtandaoni. Mfano wa huduma hizo ni Codility.com na InterviewZen zinazofanya usaili wa waandaji wa programs za kompyuta (programmers).

Kupanua uwezekano wa wapi mtu anaweza fanya kazi: 
Kutegemeana na aina ya kazi, teknohama inawezesha watu wengi kufanya kazi kazi na waajiri /wateja toka maeneo ya mbali hata nchi nyingine kabisa kwa kutumia tuu kompyuta zao. Hata kuna huduma maalum kama Freelancer.com na Guru.com zinazokutanisha waajiri na waajiriwa ambao hufanya kazi bila muajiriwa kulazimika kuenda eneo la kazi la muajiri.

Utafutaji wa taarifa :  Ukiwa kazini unaweza tumia teknohama kutafuta taarifa fulani au hata kuuliza maswali kwa watu wenye ujuzi wa mambo nao wakakusaidia. Kwa kutumia vitu kama Forums mbalimbali mfano fórums zinazowakutanisha watumiaji wa bidhaa fulani kuulizana maswali na kujibizana. Au hata kutumia website kama Quora na Stack Exchange kuuliza maswali na kupatiwa majibu. Ukiacha huduma hizi za maswali na majibu, waweza tumia huduma zilizo zoeleweka na wengi ambapo utatumia search engine kama Google , Bing, Lycos kutafuta taarifa unazotaka.

Hitimisho
Ni kweli kuwa teknohama inapanuka siku hadi siku, na ndio haswa kwas asa inayobeba uwepo na ufanisi wa mambo mengi katika maisha yetu. Kwa wale wenye kufikiria kipi wasome ili kupata ajira si vibaya wakaangalie fursa zilizopo katika teknohama na kuchagua masomo yanayohusiana na teknohama.
Ni swala lililo wazi kuwa bado kwa Tanzania watu wengi hawajafaidika na fursa nyingi zinazoletwa na teknohama, pengine kwa sababu ya kutofahamu uwepo wa fursa , pengine ni kwa sababu ya kutopata muamko wa kuanza kuzitumia, na labda zaidi sana ni matatizo ya kimiundo mbinu.

Tuamke sasa, nasi tuanze kuunda huduma na bidhaa zinazohusiana na teknohama , badala tuu ya kuwa watumiaji. 
Share:

0 comments:

Post a Comment