Watu wengi wanaamini kuna watu maalum wa kufanya vitu
fulani na tunaamin wanaofanya wana akili nyingi au imepangwa iwe hivyo
. Hata hivyo kwa kiwango kikubwa imani hiyo siyo kweli.
Mfano kuongea kingereza
kizuri mpaka usome shule nzuri au kufaulu lazima usome shule nzuri na hii ipo hata
kwa wazazi huamua kuwapeleka watoto wao shule fulani wakitumaini moja kwa
moja watoto wao watafaulu tuu. Ingawaje ni kweli shule nzuri inaweza saidia,
ila bado ukweli unabaki pale pale kuwa zinahitajika juhudi
za ziada katika kufanikisha mafanikio kwa mwanafunzi.
Lengo la mfano wa imani kuhusu shule ni kudokeza namna ambavyo tumekuwa na mazoea
ya kutotazama na kutilia maanani uwezo wa mtu , pia kufuata mkumbo au kufanya
mambo kwa mazoea.na wanafundisha vizuri lakini hajui kufaulu kunaanzia na juhudi
za mtoto wake .
Mfano huu pia una lengo la kudokeza namna ambavyo mazingira yana changia
sana kutotimiza ndoto zetu na kusema hatuwezi.
Je ufanyaje ili uanze kujiamini ?
Kuamin unaweza haitoshi kufikisha malengo, ili kutimiza haya
unapaswa kuchukua hatua na kwa kuanza kutenda ilo jambo kupangilia
mda wako vizuri, kufanyia mazoezi na kujaribu mara kwa mara
bila kuchoka wala kukata tamaa.
Unahitaji kuelewa kuwa mafanikio nikule
kutimiza ndoto zako kwa kufanya kile ambacho ulidhani hauwezi kufanya
.mafanikio yanaweza kuchukua muda, lakini kufanikiwa kunahitaji hatua kwa
hatua kwa kua mafanikio ni safari.
Hitimisho
Hivyo kumbuka wewe pia unaweza kufanya mambo makubwa sana. Unahitaji:
Kupagilia mda
Kufanya mazoezi
Kusoma vitabu na majarida kupata ujuzi zaidi
Kuwa karibu na kuomba ushauri
au msaada kwa wale wanajua au wenye uzoefu zaidi.
0 comments:
Post a Comment