Personal pronouns kwa Kiswahili Viwakilishi
vya nafsi, ni maneno yanayotumika badala ya kutaja majina ya watu, vitu,
maeneo, hali n.k
Mfano : Badala ya kusema John and Juma are
happy. (John na Juma ni wenye furaha) waweza kusema They are happy. ( Hapa THEY
, inawakilisha John na Juma ikimaanisha WAO).
Mifano mingine ya viwakilishi vya nafsi ni
HE, HIM – Yeye (Mwanaume)
SHE,HER, - Yeye (Mwanamke)
IT, - Yeye (Kitu)
THEY, THEM- (Wao)
WE, US,-(Sisi)
I , ME -(Mimi)
Baada ya
kusoma maelezo ya aina za personal pronouns utaelewa kwa nini tuna maneno
mawili tofauti ya personal pronouns kwa kila aina ya kiwakilishi hapo juu.
Aina za Personal Pronouns
Katika
sentensi vitu au watu vinaweza kuwa mtenda au mtendewa. Tunasema mtenda wa
tukio endapo mtu au kitu kinafanya tendo kwa kitu au mtu mwingine. Na huyo
anayepokea tendo toka kwa mtendewa basi anakuwa mtendewa.
Mfano
chukulia sentensi ifuatayo:
Juma
anamfundisha Aisha.
Hapa
Juma anatenda (Mtendewa) na Aisha
anatendewa (Mtendewa). Kama tukiandika kwa kutumia personal pronouns, tutapata
sentensi hii.
Yeye (mwanaume)
anamfundisha yeye(mwanamke)
He is teaching her.
Mfano huo
hapo juu unatuleta katika aina mbili za personal pronouns, yaani subject personal
pronouns, na object personal pronouns.
Subject
personal pronoun yaani kiwakilishi cha
nafsi mtenda,
na
Object personal pronoun ni kiwakilishi cha nafsi mtendewa.
Matumizi ya Personal Pronouns
Kuelewa
vema aina hizi za viwakilishi kunakuwezesha kutunga sentensi zinazoeleweka na
kukufanya uje uelewe vipengele vingine vya lugha kama kuandika Passive Voice,
yaani sentensi ambazo zinalenga kuanza kumtaja mtendewa wa tukio kwanza.
Passive
Voice ni somo pana na linahitaji uelewa mzuri wa aina za personal pronouns kama
tulivyotaja hapo juu, na pia uelewa mpana wa aina za nyakati.
Kwa kua
tumekwisha jifunza aina za nyakati za
wakati uliopo, ngoja nikudokezee walau mifano miwili ya Passive Voice uone
matumizi ya Personal pronouns
Active Voice
He teaches her.— Yeye
(mwanamme) anamfundisha (mwanamke).
Hapa mtenda
ni yeye (mwanaume) na kwakua ni mtenda, tumetumia HE, mtendewa ni yeye
(mwanamke) tungeweza kusema SHE, ila tukumbuke kuwa katika sentensi hii yeye
mwanamke ni mtendewa hivyo basi inabid tutumie HER.
Passive Voice :
Kumbuka passive voice huanza na mtendewa. Ambaye kwa sentensi yetu ni yeye(mwanamke).
Hivyo itakuwa:
She is taught by him.
Yeye (mwanamke) anamfundisha (mwanaume)
Hapa utaona kuwa
hatujatumia HER, mwanzoni kwakua tunaanza na YEYE(mwanamke) kama mtenda na
uliona hapo juu kuwa kama yeye mwanamke ni mtenda ni SHE na kama ni mtendewa
inakua HER.
Kwa
mwanaume tumetumia HIM badala ya HE, kwakua tuliona hapo juu kuwa HE ni kwa
mtenda na HIM ni kwa mtendewa.
Hitimisho
Jitest
1.You and ………….. (I, Me) are brothers. ( Wewe na Mimi ni mtu na kaka ake).
2. She has invited ………….(We,US). ( Yeye ametualika sisi)
3. They were
taught by.......... ( She, Her) Walifundishwa na yeye (mwanamke)
4.………..(He,Him) always bring his daughter here. (Yeye mwanaume daima humleta mtoto
wake hapa).
Nitumie majibu yako
kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au niachie ujumbe kwa ukurasa wetu wa Facebook,
bofya hapa kuenda kwa ukurasa wetu.
0 comments:
Post a Comment