FANYA HIVI UPATE MUDA WA KUTIMIZA MIKAKATI YAKO


Pengine una ndoto kibao za maisha, na ili kuzifikia una mikakati mingi hata hivyo siku zinaenda na hautimizi mika
kati yako. Sababu kubwa unayoifahamu ni kuwa hauna muda.
Unajiona wazi kuwa umetingwa na mambo mengi, Siku inaanza na kuisha na ukitafakari mambo gani haswa umefanya kwa ajili ya "future" yako huyaoni, zaidi ya yale uliyofanya kwa ajili ya sasa, iwe kazini, au kuenda darasani, au kuenda kwa biashara yako kufanya shughuli za kila, na sio yale mengine ambayo unajua ndio yatakayokusaidia kupiga hatua toka hapo ulipo.






Usikubali kuendelea kufanya yale yale kila siku , kwasababu hayo hayo ya kila siku, hayatoleta mabadiliko. Usiishi kwa mazoea. Ila pengine haujui uanzie wapi kupata muda na nguvu ya kufanya yaliyo tofauti.
Mfano pengine unajua kuwa kufahamu English vema ni mkakati wa lazima ili uweze kupiga hatua hapo ofisini, shuleni au kibiashara, na pengine hata umenunua kile kitabu nilichoandika kwa kiswahili kukurahisishia kuelewa vema English. Hata hivyo haujapata muda wa kuanza kusoma, ila unajiambia kipo katika mkakati, utakisoma tuu. Muda unaenda na hauoni mwanga wa lini utafanya hivyo.
Nataka ukumbuke kitu kimoja, daima hautokuwa na muda wa kutosha kwani ukweli sio kwamba watu wanafanya mambo makubwa kwa kuwa wana muda wa kutosha, bali ni kwakuwa wanapangilia VIPAUMBELE. Kinachokufanya ufanye unayofanya sasa ni kuwa hayo ufanyayo umeyapa kipaumbele. 
Hivyo angalia mambo gani uliyonayo sasa uyatoe katika vipaumbele vyako ili uingize mambo mengine unayohitaji haswa haswa yawe kama vipaumbele. Hivyo badala ya kutumia DK40 kuwa mtandaoni kusoma mambo yasiyo na msingi kwa "future" yako, tumia hizo dk40 kusoma kitabu chako cha English.
Huo ni mfano tuu wa kusoma English. Kuna mambo mengine mengi ambayo wewe unahitaji kuyafanya. Yaweke ktk kipaumbele.
Mara nyingi mafanikio yanahitaji kujua nini haswa uache kufanya. Tafakari leo , nini haswa unahitaji kuacha kufanya.
Share:

2 comments:

  1. thanks for sharing the great info

    www.clikat.com

    ReplyDelete
  2. Hakika kuweka vipaumbele kunaleta nidhamu ktk matumizi ya muda, thanks fir sharing brother.

    ReplyDelete