KULETA MABADILIKO KATIKA MAISHA YAKO AMUA HILI

Utashi wa maamuzi
Haijalishi wewe ni masikini kiasi gani, haijalishi kuwa wewe si msomi, haijalishi wewe si mtaalamu wa aina fulani, ukweli ni kuwa una kitu kikubwa na cha thamani sana ambacho hakuna anayeweza kukichukua au kukiondoa isipokuwa wewe mwenyewe.
Kama ukiitumia mali hiyo uliyonayo kwa namna nzuri basi waweza boresha sehemu maisha yako kwa kiasi kikubwa sana.
Mali hiyo ni UTASHI WA MAAMUZI.
Mfano yawezekana hauna kazi sasa, yawezekana hauna kazi nzuri, yawezekana masomo fulani kwako ni magumu. Ila pengine umekata tamaa, pengine haujiona unaweza kubadili hali. Pengine umeacha kutafuta njia mbadala ya kutoka hapo ulipo, umeshaamua bila kujijua kuwa wewe ni wa hivyo hivyo. Kuwa uliumbwa uwe hivyo.
Ila ukiamua kutumia utashi wako kufanya mabadiliko sasa. Ukafanya uamuzi wa kuamini tofauti. Ukafanya uamuzi wa kutafuta msaada, wa kujibidiisha ktk kujaribu njia tofauti tofauti , mambo yatakuwa tofauti.
Share:

0 comments:

Post a Comment