Tunapoanza kujifunza nyakati, hakikisha unazingatia kanuni
zinazoongoza nyakazi husika. Pia kumbuka kanuni zifuatazo za ujumla :
- . Kwa nyakati zote za kukamilika (zote zenye hali perfect yaani present perfect, future perfect, na past perfect) , vitendo (verbs) lazima ziwe katika muundo uitwao Past Participle.Mfano: Go – Gone (Kuenda), Eat – Eaten (Kula), Write –Written (Andika), Buy – Bought (Nunua). Tafadhali angalia document maalum ya vitendo na past participle zake.
- Kwa nyakati zote hali ya kuendelea ( zote zenye hali ya continous yaani present continous, past continous, future continous, past perfect continous, present perfect continous, na future perfect continous) vitendo vitaishia na ING.
- 3. Katika kila kila nyakati utakayosoma ni lazima ujue miundo ifuatayo MINNE ya sentensi
Sentensi ya maelezo chanya : Anaimba vizuri. He is singing well.
Sentensi ya kukanusha. Haimbi vizuri. He is
not singing well.
Sentensi ya kuuliza. Je anaimba vizuri ? Is
he singing well ?
Sentensi ya kuuliza katika kukanusha:
Je haimbi vizuri ? Is he
not singing well ?
Mifano hiyo hapo juu nimekupa katika present
continuous tense, ila kumbuka tutakapokuwa tunajifunza kila tense lazima ujue
namna ya kutunga sentensi katika hizo hali kuu nne za sentensi.
Mfano: Eat – eating (Kula), Play- Playing (Kucheza), Take –
Taking (Chukua).
Kanuni kuhusu nyakati
Wakati Uliopo ( Present Tense):
Tuanze somo
letu hili kwa kuangalia kanuni maalum zinazohusu nyakati zilipo katika kundi la
wakati uliopo, nyakati hizo ni present continous tense (wakati uliopo hali ya
kuendelea), present perfect tense
(wakati uliopo hali ya kukamilika), present perfect continous tense (wakati
uliopo hali ya kuendelea kunakokamilika).
Wakati uliopo
hali ya kuendelea (Present Continous Tense)
Kanuni
kuhusu vitendo (Verbs): Kumbuka
tulikwisha sema tenses zote za continous , vitendo huishia na ING. Hata hivyo
kabla ya kuishia na ING , hakiisha verbs zimetangulisha na IS, ARE au AM
kutegemeana na ifuatavyo:
He/She/It – IS
They, We, You – ARE
I – AM.
Mfano:
I am eating – ninakula
She is reading –anasoma (mwanamke)
He is cooking –anapika (mwanaume)
They are talking – Wanazungumza
Sasa
tuangalie namna ya kuandika sentensi katika miundo ile minne tuliyosoma sehemu
ya utangulizi
Sentensi za maelezo chanya : Hizi hutoa taarifa bila kukanusha
wala kuuliza swali. Mfano
He is
cooking – anapika.
Jinsi ya
kuandika sentensi za maelezo chanya katika
present continuous tense :
Katika
muundo wa sentensi hizi, hakikisha mtenda anatajwa mwanzoni, kisha kufuatia na
IS au ARE kutegemeana na aina ya mtenda wa kitendo kama tulivyoona hapo juu.
Mfano:
I am eating – ninakula
She is reading –anasoma (mwanamke)
Anaimba vizuri.
He is singing well.
Sentensi za kukanusha
: Hizi hutoa taarifa za kukanusha wala tukio.
Mfano
Haimbi vizuri. -He is not singing well.
Jinsi ya kuandika
sentensi za kukanusha katika present continuous tense :
Katika muundo wa sentensi hizi, hakikisha mtenda anatajwa
mwanzoni, kisha kufuatia na IS au ARE kutegemeana na aina ya mtenda wa kitendo
kama tulivyoona hapo juu halafu ifuate NO, kabla yakutaja kitendo.
Mfano: He is not
singing. –Yeye haimbi
They are not eating – Wao hawali
I am not reading – Mie sisomi
Sentensi ya kuuliza chanya: Hizi huuliza swali katika hali
chanya. Mfano
Je anaimba vizuri ? Is he singing well ?
Jinsi ya kuandika sentensi za kuuliza chanya
katika present continuous tense :
Katika
muundo wa sentensi hizi, hakikisha mtenda HATAJWI mwanzoni, Hivyo basi ANZA na
AM, IS au ARE kutegemeana na aina ya mtenda wa kitendo kama tulivyoona hapo juu
halafu ifuate MTENDA kabla yakutaja kitendo.
Mifano Zaidi: Is he
teaching ? Je anafundisha ?
Am I going to school
? Je ninaenda shule ?
Sentensi ya kuuliza katika kukanusha: Hizi huuliza swali
katika hali ya kukanusha. Mfano
Is he not playing ?
Je hachezi ?
Are we not going now ?
Je hatuondoki sasa ?
Jinsi ya kuandika
sentensi za kuuliza kwa kukanusha katika present continuous tense :
Katika muundo wa sentensi hizi, hakikisha mtenda HATAJWI
mwanzoni, Hivyo basi ANZA na AM, IS au ARE kutegemeana na aina ya mtenda wa kitendo
kama tulivyoona hapo juu halafu ifuate MTENDA, kisha malizia NO, kabla yakutaja kitendo.
Mifano:
Is he not playing
? Je hachezi ?
Are we not going
now ? Je hatuondoki sasa ?
0 comments:
Post a Comment