Kufahamu matumizi sahihi ya nyakati ni jambo la msingi sana
ili uweze kuandika na kuongea sentensi zenye kueleweka kama unavyokusudia.
Mfano angalia sentensi hii:
Jana nitakupa kitabu.
Hapa nyakati imetumika vibaya hivyo kupoteza maana , hatujui
mtu anakusudia kusema KESHO nitakupa kitabu , au alimaanisha Jana NILIKUPA
kitabu.
Hivyo hivyo katika kiingereza , usipotumia vizuri Nyakati
(kwa kizungu tunaita TENSES) basi utajikuta ukiwachanganya watu wanaosoma
sentensi zako au kukusikiliza.
Aina za nyakati
Nyakati zimegawanyika katika makundi makuu matatu:
Wakati uliopo ( Present Tense)
Wakati Ujao (Future Tense)
Wakati Uliopita ( Past Tense)
Hata hivyo matukio yote iwe wakati uliopita, uliopo au ujao,
yanaangukia katika HALI zifuatazo:
Hali ya
kuendelea (Continous)
Hali ya
kukamilika (Perfect)
Hali ya
kawaida (Simple)
Hali ya
kuendelea kukamilika ( perfect continuous)
Hivyo basi
tunaweza kuwa na aina hizi za tenses
Wakati Uliopo: (Present Tnese)
Simple
Present Tense( Wakati Uliopo Hali ya Kawaida)
Present
Continous Tense (Wakati Uliopo Hali ya Kuendelea)
Present Perfect Tense( Wakati Uliopo Hali ya Kukamilika)
Present Perfect Continous Tense( Wakati Uliopo Hali ya
Kuendelea Kukamilika)
Wakati Uliopita:
(Past Tense)
Simple Past Tense( Wakati Uliopita Hali ya Kawaida)
Past Continous Tense (Wakati Uliopita Hali ya Kuendelea)
Past Perfect Tense( Wakati Uliopita Hali ya Kukamilika)
Past Perfect Continous Tense( Wakati Uliopita Hali ya
Kuendelea Kukamilika)
Wakati Ujao: (Future
Tense)
Simple Future Tense( Wakati Uliopita Hali ya Kawaida)
Future Continous Tense (Wakati Uliopita Hali ya Kuendelea)
Future Perfect Tense( Wakati Uliopita Hali ya Kukamilika)
Usikose masomo yanayofuata
shukran
ReplyDelete