SOFTWARE INAUTAFUNA ULIMWENGU : JE UNASHIRIKI VIPI ?

software unashiriki vipi
photo by dreamstime.com
Mara ya mwisho lini ulituma au kupokea barua kwa njia ya posta ? Unajiuliza masaa mangapi kwa siku unatumia ukiwa mtandaoni ? Je kuna mwanafunzi walau tuseme wa ngazi ya chuo ambaye kwa sasa anasoma bila kutumia mtandao hususani Google kutafuta madesa ?
Wangapi kati ya rafiki zako hawatumii WhatsApp au Facebook ?
Mara ya mwisho lini ulitembelea ofisi kubwa ya serikali au binafsi usikute kompyuta ?
Tumeshazoea uwepo wa software ktk maisha yetu kiasi kwamba hata tumesahau , kuwa kuna wakati ilitubidi tusubiri saa mbili kasoro usiku kusikiliza michezo kujua matokeo, ila sasa ni moja kwa moja kupitia tv au magrupu yetu ya FB na WhatsApp.
Hii tuu ni namna ya rahisi ya kuelezea jinsi Software zinavyogusa maisha yetu ya mtu wa kawaida.
Kwa mtazamo wa juu kidogo, kuna mambo ya kiafya, tafiti, uzalishaji, na usalama ambayo bila software , hayotoweza kufanyika.
Hata hivyo , nina mashaka kama sisi watanzania tumeandaliwa vya kutosha kushiriki katika kuzalisha hii mifumo na bidhaa zinazoleta mabadiliko na kuboresha maisha.
Je kwa kiwango gani shule zetu au mfumo wetu wa elimu na uchumi unatilia maanani kuwezesha watu kujikita katika sayansi ya kompyuta ?
Je, miundo mbinu yetu kama upatikanaji wa umeme na huduma ya internet inasaidia watu kujifunza na kufanya kazi katika shughuli za mambo ya sayansi ya kompyuta ?
Je watu wetu wanatilia maanani kiasi gani ujuzi wa lugha ya kiingereza ambayo ndio msingi mkuu wa kujifunza mambo ya sayansi ya kompyuta na kushirikiana na wadau wengine wakubwa katika fani hii ?
Share:

0 comments:

Post a Comment