JE GEEKS, NERDS, HACKERS NI WATU WA AINA GANI ?

geeks_nerds_hackers
picha na Huffingtonpost
Leo tuangalie maneno haya geeks, nerds, na hackers ambayo yamekuwa maarufu katika mitandao hususani siku za hivi karibuni, na wengine kuyatumia isivyo sahihi.

Geeks ni watu wa aina gani ?
Bila shaka umewahi ona watu kadhaa wakijiita GEEKS, na mara nyingi watu hawa huwa katika fan iza kompyuta, fizikia, hesabu au sayansi kwa ujumla. Hata hivyo neno hili sio tuu litumike kwa watu wa fani hizo. Neno geek kwa tafsiri toka Wikipedia,  kwa matumizi maarufu ni kuwa mtu mwenye mapenzi makubwa katika somo fulani au fani fulani na mali somo au fani husika huonekana ngumu kwa watu wengi.  Kwa sababu ya mapenzi yao makubwa katika somo husika, watu hawa hutumia muda mwingi kujifunza na kufanyia kazi matatizo katika somo/fani husika kiasi kwamba huwa ni “wazuri” sana katika somo/fani husika.
Hivyo kabla haujajiita wewe ni GEEK katika swala/somo fulani hakikisha kuwa swala hilo kwanza kwa ujumla ni gumu sana, halafu wewe umewekeza muda mwingi katika kujifunza mambo ya hilo swala/somo, na kwamba una uelewa mkubwa na mapenzi makubwa ya jambo husika.
Nerds ni watu wa aina gani ?
Kwa ujumla wake, nerds hawana utofauti sana na geeks. Hata hivyo neno geeks hutumika kuwaelezea watu waliojikita Zaidi katika somo/swala moja na wanajishughulisha na hilo tuu kwa muda mrefu. Wakati nerds mara nyingi huwa wanajikita katika mambo Zaidi ya moja na kutafuta kupenda na kuweza vitu tofauti.
Nerds hutambulika pia kwa kutokuweza kwao kujishughulisha na mambo ya kijamii kama vile kutokuweza kuvaa mavazi mazuri au ya kisasa, na kuwa na hobbies ambazo ni za “ajabu” machoni mwa wanajamii wengi.
Kwa kiwango cha undani wa kujifunza nerds hujikita ndani Zaidi katika wanayoyasoma ili sio tuu kuweza kutengeneza au kutumia kitu fulani , bali wafahamu ndani  na nnje ya kitu husika.

Hackers ni watu wa aina gani ?
Katika ulimwengu wa fani ya usalama wa mifumo ya mawasiliano, hacker ni mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu katika maswala ya programming na mifumo ya kompyuta. Katika maana hii tunaambiwa kuwa kwa sababu ya ujuzi wao mkubwa wa maswala ya programming na mifumo ya mawasiliano, hackers huweza kuunda mifumo na programs kwa haraka na zenye kuleta tija.

Hata hivyo, kama ilivyo katika kila kitu duniani, kuna faida na hasara zake. Wapo watu wanaotumia ujuzi wao mkubwa wa programming na kujua mifumo ya mawasiliano kuichambua na kufanya uhalifu, na kwa bahati mbaya habari mbaya ndio husambaa zaidi kuliko nzuri, hivyo watu wengi wamekua wakiamini hackers ni watu waharibifu wanaoingilia programs na mifumo ya mawasiliano kuleta hitilafu na kuiba taarifa.
Share:

0 comments:

Post a Comment