Je
unajiuliza uanze wapi ili kufikia ndoto zako za maisha ya kimataifa iwe kufanya
kazi nje ya nchi, au kuwa na ushirikiano na watu wa mataifa mbalimbali. Katika
makala hii naeleza mambo ya msingi ya kuzingatia ili uweze kuwa mshirika wa
jumuiya ya kimataifa yaani uweze kuwa na marafiki na washirika toka mataifa
mbalimbali katika shughuli zako halali za kila siku. Mambo haya ninayoeleza ni kwa uzoefu wangu na
kujifunza toka kwa watu wengine, kitu tunachoita international exposure, yaani
uzoefu wa kimataifa kwa kutembea na kuishi nchi tofauti tofauti.
Tamaduni za kuacha:
Kuna mambo
kadhaa umejizoesha kuyafanya na ingawa twajua wazi si sahihi na yanakera
wengine bado tunaendelea kuyafanya kwa kisingizio tuu eti hivyo ndivyo tulivyo.
Ninasema twajua yanakera kwakuwa sisi tukifanyiwa mambo hayo hayo yanatukera.
Mfano endapo utamuambia mtu utafanya kitu fulani, kisha usifanye kwa sababu
fulani pengine ya kusahau au kutotilia maanani, wajua wazi kua hata wewe
usingependa kutegemea jambo toka kwa mtu halafu mtu huyo asikufanyie.
Katika
maisha ya kimataifa , ustaarabu ni kuthamini muda wa wengine, ni kuwajali
wengine na kufanya mambo unayoahidi utafanya. Na kama hautoweza kufanya, basi
utoe taarifa kwa wakati muafaka kuwa hautoweza.
Kuwa
muwazi, mkweli na kuwajibika katika jukumu unalotarajiwa kufanya ni mambo
yanayotarajiwa kutoka kwako ili uweze kufiti kuishi na watu wa mataifa tofauti
wenye kuweza kushirikiana nawe kufika mbali kimaisha.
Uwezo wa kufikiri kwa akili ya kawaida na
kubadilika
Kuna mambo
mengi tunaamini na kufuata bila kufikiria sisi wenyewe. Pengine unafuata na
kuamini mambo fulani sababu tuu ulisoma hivyo darasani, watu wengi wanaamini
hivyo basi itakuwa ni sahihi, au kwakuwa watu fulani wenye vyeo, watu maarufu
wa wakubwa kwako ki umri wanasema hivyo. Uwezo wako kuwa salama na kufanikiwa
katika maisha ya kimataifa unahitaji sana uwezo wako binafsi wa kufikiri na
kufanya maamuzi kwa kupima maelezo kwa akili yako ya kawaida tuu (common
sense).
Utakutana
na watu wengi wenye malengo tofauti hivyo utapata mitazamo na taarifa tofauti.
Hautotakiwa kuamini zote, utatakiwa kuchuja wewe mwenyewe na kufanya maamuzi
yenye manufaa kwako. Jifunze sasa kuhoji mambo, chunguza maamuzi yako na
ujihoji hadi wewe mwenyewe . Tafuta taarifa zaidi ya unayoamini kuwa ni ukweli,
unayosikia, na ukubali kuwa tayari kubadilika kimtazamo endapo utakuta kuwa
ulichokuwa ukidhani ni sahihi sikuzote kumbe sio.
Uwezo wa kufanya mawasiliano
Nimeongelea
sana umuhimu wa kujua kufanya mawasiliano kwa ufasaha na namna ya kufanya
mawasiliano katika makala FANYA HIVI KAMA UNATAKA KUPATA UFADHILI WA MASOMO AU MTAJI WA BIASHARA Tafadhali bofya HAPA kusoma makala hiyo.
Ujuzi wa lugha
Pointi hii
haihitaji maelezo kufafanuliwa sana kwani bila ujuzi wa lugha ya mawasiliano,
hakuna kitu utaweza kufanya katika ulimwengu wa kimataifa, haijalishi uwezo
wako wa kielimu, au bidii zako kikazi. Fahamu lugha kuu ya mawasiliano yaani
Kiingereza.
Umuhimu wa ndoto
Ninaposema
ndoto ninamanisha uwezo wako wa kufikiria na kutumaini mambo makubwa, sio ndoto
zile za usingizini. Uwepo wa ndoto
unakufanya utengeneze mwelekeo wa namna gani maisha yako unatakiwa uyaendeshe
sasa ili kufikia huko unapotaka kuenda. Mfano kama unaota kuwa siku moja uende
kufanya kazi nje ya nchi, basi bila shaka utaanza sasa kujifikiria namna gani
ya kujiimarisha katika lugha ya kigeni na pia kuanza juhudi za kupata taarifa
zaidi kuhusu maisha nje ya bongo. Usipokua na ndoto, basi utajichukulia poa na
hivyo kutofanya juhudi sana.
Kuwa karibu na mtandao (Internet)
Matumizi ya
mtandao ni zaidi ya kutumia Facebook , Instagrams, Blogs na WhatsApp. Baadhi ya watu huishia kutumia simu zao kwa
ajili ya mitandao ya kijamii, na wakizidi sana watatumia Google kutafuta
taarifa fulani. Maisha ya kimataifa
yanakuhitaji uwe na uzoefu na taarifa tofauti tofauti nyingi kuhusu mataifa –siasa
, uchumi, tamaduni, teknolojia na matukio makubwa. Na zaidi sana uwe na taarifa
sahihi au zinatoka kwa vyombo huru na vya kuaminika na sio toka kwa watu wanao
copy na kupaste kwa blogs zao au kwa akaunti zao za FB bila kufanya utafiti.
Kuwa na
taarifa sahihi na kuzashare kunakufanya uaminike na kuonekana mtu sahihi wa
kushirikiana katika mazungumzo.
Pia
jizoeshe kutumia email kwa mawasiliano na mara kwa mara ufungue na kutumia
akaunti yako ya email.
Asante sana ndugu
ReplyDeleteAsante sana ndugu
ReplyDeleteAsante sn. Ila ninaombi na pia ushari nahitaji kwasababu nimemaliza kidato cha nne na nimefaulu kwenda chuo ila wazazi hawana uwezo wakunipeleka kbc ilikuwa niripot chuo 5/9/21 ila kwasababu ya kukosa ada na matumizi mengine nipo nyumbn mpk sasa. Na nimejaribu kufanya fanya vikazi ili hata nianze kujinunulia vitu vidogodogo vya chuo. Nilikuwa naomba msaada unisaidie nitapataje wafadhili wanifadhi ili nikasome nahitaji kusoma Sana ila ndio hivyo. Naitwa Hellen elinaz naishi arusha 0693368655. Nitafurahi sn Kama nikisaidiwa na MUNGU awabariki katika majukumu yenu ya kila siku.
ReplyDeleteNaomba MSAADA wa masomo Mimi ninasoma Engineering nimekwama Ada na mahitaji mengine naomba MSAADA niweze kusoma
ReplyDeleteEmail lizycha7@gmail.com
0688822449/0787510645
Naitwa Ali naomba
ReplyDeleteMsaada.wenu tafadhali
Nimemaliza
Kidato.cha sita.mwaka2020
Hadi
Nimeshindwa
Kuendelea
Namasomo.yachuo
Kikuu
Kutokana
Na
Hali
Mbaya
Ya
Uchumi
Wafamilia
Yangu
0675676575