Utangulizi
Imewahi
kusemwa kuwa ‘You are what you think’ , yaani unavyofikiri ndivyo utakavyokua.
Hii ni kweli hata katika mahusiano. Namna tunavyofikiri kuhusu sisi wenyewe na
aina ya wapenzi tunaowataka ndivyo inatupelekea kuwa katika mahusiano machungu
au ya furaha.
Katika
makala hii nazungumzia baadhi ya sababu au malengo ya kuingia katika uhusiano
ambayo huchangia watu kujikuta kuwa katika mahusiano machungu.
Mwanamme anataka mwanamke wa aina gani ?
Kwa baadhi
ya wanaume mwanamke ni kama mfanyakazi wa ndani –ila zaidi ya mfanyakazi ni wa
kuwazalia watoto na kulea. Kwa wengine ni chombo cha starehe,wakitilia maanani
uzuri wa sura na umbo.
Mwanamke anataka mwanaume wa aina gani ?
Kwa baadhi
ya wanawake , mwanaume ni tiketi ya 'kutoka ' kimaisha. Ni mlezi baada ya baba na
mama yao. Mwanaume ni wa kumrahisishia maisha na kumfanya apumzike kuwaza na
kuhangaika katika mihangaiko ya kila siku.
Na bahati mbaya
wapo wanawake wengi huingia katika mahusiano ambayo wanajua wazi wao hawawezi
kuwa washirika wa kweli wa waume zao. Ila wanaona ni poa kuwa hawataki
shida, kwani anaonekana mwanaume anao uwezo wa kumtunza na kumrahisishia maisha.
Wanawake wa aina hii wanaangalia upande mmoja tuu wa mahusiano, yaani namna gani wao
watanufaika kwa ‘kulelewa’ vizuri na
mume, na sio kwa namna gani wao pia watakua wa msaada kwa mwanaume husika –msaada
kimawazo, kimazungumzo, na haswa haswa kwa ndoto ambazo mwanaume ameweza kushea
nae.
Matokeo ya malengo mabaya ya aina ya mwenza
unayehitaji
Kwa watu wa
mtazamo wa hivi, wanajikuta wakiingia katika mahusiano bila muunganiko haswa wa ushirika unaowafanya kuwa
mwili mmoja kwa mpangilio wa maisha ya mapenzi yenye furaha na hatimaye ndoa yenye furaha.
Hivyo watu wanaanza mahusiano na kuingia katika ndoa ,
lakini kiukweli hakuna ushirikiano na umoja unaotakiwa wa maisha ya furaha.
Mwanaume akijua wazi kuwa hana mshirika anakubali kuingia katika ndoa pengine
kwa misukumo ya kifamilia, au kwa sababu anazoona za ‘kiusalama’ kuwa kwa kuwa
na mke wa hivyo , yeye atakuwa na nguvu sana juu yake, hivyo hakutakuwa na
sababu ya mwanamke kutoka nje ya ndoa, na yeye mwanaume atakua na uhuru wa ‘kucheza’.
Pengine mwanaume aliumizwa katika mahusiano
yake yaliyopita wakati hana uwezo wa kifedha au hakuwa na sauti katika
mahusiano hivyo anajiona njia ya kuwa salama ni ya kuwa na mwanamke ambaye wana
‘gepu’ kuwa na yeye ndo atasikilizwa.
Kutokuwepo kwa usawa au ushirikiano wa karibu kama washirika
katika mahusiano au ndoa, kunafanya wawili hao ingawa wapo pamoja muda mrefu ,
pengine wanaishi nyumba moja , wakawa wako mbali kimauhisano kwakua ‘hawazungumzi
lugha moja’.
Wapenzi wanakuwa na mahitaji mengi ambayo hayakamilishwi na uhusiano walio nao,
na uvumilivu wa kukubali kutokukamilika huko ni mgumu hivyo anayeumia zaidi kwa
kutokukamilika mahitaji yake, anatoka nje ya uhusiano ili kuziba pengo.
Hata hivyo kutoka huko hakuleti furaha ya kweli kwa muhusika
kwani tayari amekwishajikomit kwa mwenza fulani, kinachoendelea ni kua wakati
akitafuta furaha ya muda mfupi, anasababisha maumivu makubwa kwa mwenza wake na
kwake mwenyewe, na pengine kwa watoto kama wana watoto.
Hitimisho
Una muda
mrefu wa kuchagua na kumchunguza mwenza unayemtaka. Usikubali kuingia kwa
mahusiano ya kudumu na mtu ambaye baada ya kujichunguza wewe mwenyewe unaona
kabisa si mshirika unayehitaji. Usilazimishe mahusiano kwa kuangalia ‘faida’ na
nafasi ya mtu fulani.
Kuvutiwa
kihisia za kimapenzi na kufanya mapenzi hakutoshi kukujulisha kuwa unampenda
mtu.
Na hata kama unampenda , kumbuka muda mwingi wa uhusiano wenu mtautumia
bila kufanya mapenzi au kuwa karibu kihisia.
Unahitaji kumkubali mwenza wako
zaidi ya unavyomkubali kimapenzi.
0 comments:
Post a Comment