Picha na RT.COM |
Jana dunia imeshuhudia umahiri wa hali ya juu toka kwa mtoto wa maiaka 15 aitwae Yulia Lipnitskaya, Mrusi aliyeshinda medali ya dhahabu ktk mashindano ya kuteleza kwenye barafu.
Kuna wakati Yulia aliweza kunyanyua mguu wake mmoja na kutengeneza umbo la namba moja huku akiendelea kuteleza, na wakati mwingine alipinda kutengeneza umbo la herufi L, na akizunguka kwa kasi.
Kinachovutia kuhusu YULIA ni kuwa mama yake kwa kuamini kipaji cha binti yake, aliamua kuacha kila kitu katika mji waliokuwa wakiishi zamani na kuhamia Moscow wakati Julia akiwa na Miaka 10 ili tuu ampe "sapoti" binti huyo.
Na kweli sapoti ya mama imezaa matunda kwani Yulia amekuwa bingwa wa Urusi, bingwa wa Ulaya mwaka 2014, na amewahi kuwa bingwa wa dunia wa mashindano ya World Junior Championship mwaka 2012.
Na jana amekuwa ndio mtereza kwenye barafu mwenye umri mdogo zaidi kwa nchi ya Urusi kupata medali ya dhahabu ktk mashindano ya Olympic.
Na jana amekuwa ndio mtereza kwenye barafu mwenye umri mdogo zaidi kwa nchi ya Urusi kupata medali ya dhahabu ktk mashindano ya Olympic.
JE UNATAMBUA KIPAJI CHA MTOTO WAKO ? UPO TAYARI KUKIENDELEZA ?
Maelezo haya ni kwa uchambuzi toka RT.COM, Wikipedia na Buzzfeed.com
0 comments:
Post a Comment