JIFUNZE KIINGEREZA SOMO LA 7



Katika somo lilipita tulijifunza kanuni zinazohusu wakati uliopita hali ya kawaida ( Simple Past Tense)

Somo la leo litahusu zaidi namna ya kutumia nyakati hii muhimu katika mazungumzo yetu ya kila siku.

Matumizi  makuu ya Simple Past Tense ni kama ifuatavyo:-

1. Kuelezea matukio yalitokea ndani ya kipindi Fulani muda uliopita.

Mfano:

 Mwaka 2010 nilifanya kazi benki kuu.  --In 2010 I worked for the central bank.

Nilisoma kifaransa kwa miaka mitano.-- I studied French for 5 years.

2. Kuelezea tabia zilizowahi kuwepo hapo zamani

Muhimu kutumia maneno kama Always (daima), Often (mara nyingi), Usually (mara nyingi)

Mfano:   

Mara nyingi ni mimi ndiye niliyepika chakula. -- I often cooked food.

Daima nilikujali wakati tulipokuwa pamoja.--- I always cared for you when we were together.


3. Kuelezea mambo ambayo hapo kabla yalikuwa kweli

Mfano

Tulikuwa tukila ugali kila asubuhi kabla ya kuenda shule. ---We ate ugali every morning before going to shool.

Hakuwa mfanyabiashara maarufu mwaka jana. ---He was not a famous business person last year.

Share:

2 comments: