Kanuni
za kukumbuka
Hakikisha vitendo vyote vimebadilishwa ili kuwa
katika hali iliyopita. Mfano:
Kucheza ( tafsiri: –Play )– (Wakati uliopita: Played)
Kula – ( tafsiri: Eat )– (Wakati uliopita: Ate)
Andika-( tafsiri: Write) - (Wakati uliopita: Wrote)
BOFYA HAPA na HAPA kupata orodha ya vitendo na namna jinsi ya kuandika past tense zake.
Hata hivyo
kama unauliza swali au kukanusha, hautakiwi kuweka vitendo katika PAST TENSE,
hivyo weka vitendo katika hali ya kawaida.
Mfano : Jana sikula ugali.
Sahihi:
Yesterday I did not eat ugali.
Isiyo sahihi:
Yesterday I did not ate ugali.
Mfano: Je jana ulicheza mpira ?
Sahihi: Did
you play football yesterday ?
Isiyo sahihi:
Did you played football yesterday ?
Kumbuka:
Kuuliza swali
la wakati uliopita hali ya kawaida, ni vema kuanza na neno DID.
Mfano:
Je ja ulicheza mpira ? -- Did you play football yesterday
?
Kukanusha
sentensi ya wakati uliopita
Sikucheza mpira jana – I did not play football
yesterday.
Umeona hapo juu katika kukanusha, tunatumia DID NOT na hiyo DID NOT ni lazima
ikae kabla ya kitendo yaani kabla ya kitendo PLAY, na kwamba vitendo vyote kama
unakanusha basi hautovibadili katika past tense, badala yake vitabaki kuwa vya
kawaida.
Hizo hapo juu
ni kanuni muhimu za kujua ili uweze kutumia lugha ya kiingereza.
Somo
litakalofuata utajifunza ni wakati gani au kwa namna ipi utumie SIMPLE PAST
TENSE.
0 comments:
Post a Comment