JINSI YA KUJIFUNDISHA ADABU YA MUDA


Ingawa ni kweli kuwa hakuna kanuni ya jumla ya nini ufanye ili ufanikiwe, kumbuka kuna tabia za jumla za watu waliowahi kufanikiwa.

Mojawapo ya muongozo katika kufikia mafanikio unayotamani ni :-
Kutambua wazi wazi ni shughuli gani za muhimu kwako.
Halafu ukazipa kipaumbele hizo shughuli muhimu kwako
Ninaposema kutambua wazi wazi nina maana kuwa kwanza uchukue muda wa kutafakari maisha yako kipindi na kipindi kwani maisha yanabadilika na wewe mwenyewe unabadilika kitabia na kitafakari. Ikiwezekana weka malengo yako katika maandishi.
--Kisha tambua ni shughuli gani unazotakiwa kufanya kufikia malengo hayo, weka bayana sio tuu shughuli gani au mambo gani unatakiwa kufanya, bali pia ujue ni wakati gani unatakiwa kufanya.
--Halafu ujidhibiti wewe mwenyewe kwa kuwa na nidhamu ya kufanya hayo tuu ya msingi kwa wakati husika. Mfano kwa wanafunzi kama upo chuoni, wajua wazi jambo la kwanza kabisa la msingi kwako ni kupata uelewa na maksi nzuri, iweje uwe mtu wa kufuata mkumbo wa mambo mengine yanayokukosesha muda wa kujisomea vema ?
--Kama unafanya kazi basi unajua wazi pengine lengo lako ni kufanya kazi husika kwa muda tuu, kisha ukajiajiri. Iweje ujiingize kwenye majungu na uvivu, na kufuatilia mambo yasiyokujenga kupata ujuzi na uzoefu wa kutosha kuja kujiajiri ?
---Swala la kukumbuka nini haswa la msingi unatakiwa kulifanya au kulipata kwa wakati husika huwashinda wengi. Unakuta umeenda ofisi ya watu, ndio una haraka lakini la msingi zaidi ni wewe upate huduma yao. Kwa sababu ya ubovu wa huduma kwa mteja pengine hawakuhudumii vema, unaanzisha zogo, halafu unaamua kuondoka. Kuondoka kwako kunakugharimu zaidi, ila unajipa moyo eti "UMEWAFUNDISHA ADABU". 
Ingawa kulalamikia huduma mbovu ni jambo la msingi , lakini halikuwa jambo la kupewa kipaumbele na wewe. Kama ulitaka kuwafundisha adabu kwa kuanzisha zogo na kutimka ungeeandaa siku maalum ya kufanya hivyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment