Jionee hapa :-
1. Yale yasiyowezekana : Kusoma kunaibua ufahamu wa mambo mengi ambayo
pengine ulidhani hayawezekani. Mfano, kama ulidhani si rahisi kuwa mtu wa
maisha ya furaha katika mahusiano, baadhi ya makala unazoweza kusoma mtandaoni
zitakuonyesha njia zinazoweza kukusaidia kutambua mbinu za kuboresha uwezo wako
wa mawasiliano, uwezo wako wa utambuzi wa mahusiano bora na utajikuta unajua
uanze wapi. Mfano mwingine unaweza kudhani kuwa wewe hauwezi kuwa na kuendesha
blogu, ila baada ya kusoma makala fulani hapa mtandaoni ukajikuta unaweza kuwa
na blogu ‘kali’ sana.
2. Mambo yanabadilika:
Mengi unayodhani yapo sahihi , pengine hayapo sahihi kwa sasa. Pia mazingira,
ufahamu wa watu wengine, teknolojia, hali ya uchumi na kisiasa zinabadilika kwa
kasi sana. Hii inaathiri ufanisi wa asasi mbalimbali, na hata ufanisi na
ushindani wako katika soko la ajira na ujasiriamali kwa ujumla. Bila
kujiboresha mara kwa mara katika kujifunza mambo mapya, unaweza kujikuta upo
nyuma ya wakati.
3. Fursa mpya: Mabadiliko
na maendeleo yanayoendelea kutokea yanaleta fursa mpya zaidi kwa kila mmoja
wetu. Kujisomea kwako kutakuwezesha kutambua fursa husika, na njia sahihi za
kuzitumia. Mfano, wajasiriamali wengi wameweza kujitangaza sasa kupitia
Facebook kwa kufungua Facebook Fan Page. Hata hivyo, wachache walioweza
kujifunza kwa undani namna bora za kutumia pages hizo ndio wamenufaika, wakati
wengine pages zimekuwa kama ‘mapambo’ tuu.
4.Fursa zaidi: Hata
kama unadhani umefanikiwa sana kimaisha, haina maana kuwa hauwezi kufanikiwa
zaidi. Hata kama unadhani una kiwango cha elimu cha kutosha, bado waweza
jifunza na kuongeza fursa nyingi za kimaisha, hata kama si kwako binafsi bali
kwa wengine wanaokutegemea. Kuna fursa za kuongeza mtandao wako, fursa za
kufanya biashara zaidi, fursa za ajira bora zaidi n.k. Haya yanawezekana kwa
kuboresha ufahamu wako siku hadi siku.
5. Ufumbuzi wa matatizo:
Usikae na tatizo kimya kimya, au ukategemea tuu watu wengine wakutafutie
ufumbuzi wa tatizo, liwe la kijasiriamali, la kikazi, la kimapenzi, na hata kidarasani. Tumia vyanzo mbalimbali
vya ufahamu hapa mtandaoni kujua mengi yanayoweza kukupa mwanga wa ufumbuzi wa
matatizo yako.
6. Uhuru wa fikra: Kuna
makala nyingi kutoka kwa asasi na watu binafsi ambazo zinaeleza namna
unavyoweza kuwa huru kifkra. Vile ambavyo unaweza kutumia utashi wako kwa
ufasaha, bila kuogopa watu wengine. Utaweza pia kujifunza namna bora ya kufanya
maamuzi kwa sababu za msingi sio tuu
kukurupuka, au kufanya kwa kupendeza watu.
THANKS VERY much guys this page will be açepted to th people
ReplyDelete