IPI BORA UTASHI WAKO AU SHERIA ?

Sisi binadamu tumepewa uwezo wa kutafakari na kutambua mabaya na mazuri.
Kanuni rahisi ya kujua kama  jambo ni baya au zuri ni kujiuliza kama ingekuwa linakutokea kwako ungejisikia vipi, au kama ni wewe ndiye ungekuwa huyo mtu mwingine ungejisikia vipi.
Ni kanuni moja rahisi sana, lakini pia ni ngumu kwa kuwa:-
1. Huwa wengi hawawazi kujiweka nafasi ya mtu mwingine. Yaani kwa haraka kufikiria kama ni wewe huyo mtu mwingine unayemtendea jambo ingekuwaje?
2. Haujajingea uwezo wa kufikiri mambo wewe mwenyewe na kujiamini katika maamuzi yako. Mengi unayoamini na kuamua ni kwa kufuata mtazamo wa kanuni ambazo tayari umeshawekewa na watu wengine. Unapima zaidi uhalali wa jambo kwa kuangalia kanuni au sheria zilizowekwa kuliko kuamini katika usahihi au jambo kutokuwa sahihi kwa kujilinganisha na wewe mwenyewe kama ungekuwa ndio mhusika wa kutendewa jambo hilo.
3. Wakati mwingine unakuwa mtu wa ajabu kweli kweli eti unaogopa kutenda kwa usahihi hata kama unajua ulitakiwa kutenda kwa usahihi, kwakuwa tuu unadhani hautopata malipo sawa sawa toka kwa mtu husika (Yaani mtu husika hatokuwa mwema kwako utakapohitaji msaada wake).
Hivyo unajikuta pamoja na kujua usahihi, bado unaamua kwa makusudi kufanya isivyo sahihi. Na zaidi sana unafanya hivyo kwakufuata tuu mkumbo au maneno ya watu wengine, unaacha kusikiliza sauti yako toka moyoni inayokutaka utende kwa usahihi.
Share:

0 comments:

Post a Comment