Tafakari yetu leo
inahusu hadithi maarufu ya CHURA.
Mwanasayansi toka ujerumani Heinzmann,
aligundua kuwa chura akiwekwa kwenye chombo tuseme sufuria yenye maji baridi , halafu maji hayo yakaanza
kupashwa moto kidogo kidogo , basi chura huyo wala hatohangaika kutoka kwenye
maji, na hatimaye kufa wakati maji hayo yatakapokuwa ya moto kweli kweli.
Ingawaje kuna mabishano ya kisayansi kuhusu usahihi wa madai ya Heinzmann, leo
utajifunza kitu kuhusu habari hii ya chura.
Kumbuka ukimweka chura
kwenye maji ambayo tayari ni ya moto , atakurupuka haraka. Utafiti nilioleza hapo
juu ni kama utamweka kwa maji ya baridi.
Mara nyingi ili binadamu akubaliane kwa urahisi na mabadiliko, basi
mabadiliko hayo ni lazima yafanyike kidogo kidogo kama hiyo habari ya chura.
Jamii yetu inaporomoka kimaadili siku hadi siku, kiwango cha elimu
kinashuka na hata ufanisi makazini ni ishu. Hata hivyo matatizo hayo ya mfumo
wetu wa maisha hayajaanza leo, hayakuwa
makubwa kiasi hiki kipindi kirefu kilichopita,
ila yameendelea kukua kidogo kidogo kama vile yale maji yanavyoongezwa
joto ili kumuunguza chura. Hatukusikii wala hatuoni ni shida, tumebaki
kulaumiana ila mbaya zaidi kama vile yule chura, bado hatuchui hatua ya kujikwamua kwa haraka kwa kuwa ni kama tumekwishajizoelea hali hii.
Bado unayo nafasi ya kuamka, na kubadili kile kinachokukera. Usikatishwe
tamaa na mfumo mzima wa maisha ya jamii, mabadiliko ya kweli ya jamii
hayategemei wote sisi kubadilika kwa wakati mmoja. Kila mmoja wetu akibadilika
kidogo kidogo jamii itafika mbali.
0 comments:
Post a Comment