UKWELI KUHUSU UGUNDUZI WA ISAACK NEWTON NA KUANGUKIWA NA TUNDA

Kuna hadithi maarufu ya mwanasayansi maarufu Sir Isaack Newton, isemayo kuwa akiwa amekaa siku moja chini ya mti alidondokewa na tunda aina ya Apple, akaamua kulirusha tena juu ila Apple hilo likarudi chini.  Ndipo katika kujiuliza uliza sana akapata jibu kujua kumbe ni kwa sababu ya nguvu ya mvutano ya dunia. Ingawa ukweli wa hadithi kwa mujibu wa Newscientist.com ni kwamba Sir Isaack Newton hakudondokewa na tunda hilo, kwani katika historia ya maisha yake, moja ya mambo aliyomueleza mwandishi maalum aliyeandika historia yake ni kuwa yeyé Isaack alikuwa tuu akipita shambani na akashuhudia tunda hilo likianguka, alijiuliza maswali hayo kisha akagundua hicho alichogundua.

Ugunduzi mwingi umefanywa kwa mtindo huo, tafuta hata kujua jinsi kanuni ya Paisagorasi (Pythagoras theory) ile kanuni maarufu ihusuyo pembe tatu.

Lengo la kukudokeza hadithi hizi ni kukumbusha umuhimu wa wewe pia kuwa mtazamaji wa mazingira, kujifunza mambo yanavyobadilika, kisha kuwa na mtazamo mpya. Wengi bado wanaamini yale yale waliyokariri toka babu na babu bila hata kuhoji. Aina ile ile ya msosi, kuvaa, jinsi ya kugharamia maisha yao n.k. 
Sio lazima uwe unataka kugundua kitu, ninachotaka kukuambia hapa ni kuwa kujiuliza uliza kuhusu mambo, kuwa mtazamaji makini, na kukusanya taarifa ili kuunganisha mambo ni muhimu hata kwako ili uweze kujikwamua kutoka katika utumwa wa kifikra. Jifunze mambo mengi sio kwa sababu tuu unataka kumeza kama yalivyo, bali tafakari zaidi na ulinganishe mambo yanavyoenda. Ulichoamini jana pengine sio sahihi leo.

Nikuache na maneno haya

Anthony Robbinson: 

“If you do what you've always done, you'll get what you've always gotten. ”“Kama utafanya yale yale ambayo umekuwa ukifanya siku zote, utapata yale yale ambayo siku zote umepata”

Albert Einstein:

“Imagination is more important than knowledge. For knowledge is limited to all we now know and understand.”“ Kufikiria kwa kujenga ufahamu mpya ni muhimu Zaidi kuliko ufahamu. Kwakuwa ufahamu una kikomo kwa yale ambayo tunajua na kuyaelewa sasa.” 
Share:

0 comments:

Post a Comment