Kwanza
kabla hatujaenda mbali tambua yafuatayo:
- Sio lazima mwenye biashara awe msomi ili biashara iendeshwe kisomi
- Sio kila msomi anaweza endesha biashara kisomi.
- Kuendesha biashara kisomi sio tuu kufanikisha biashara ipate faida.
- Kuendesha biashara kisomi ni zaidi ya elimu ya darasani ya biashara
Endelea
kusoma ufahamu vizuri nini cha kufanya ili biashara iendeshwe kisomi.
Ipo
hivi, kuendesha biashara kisomi ni pale
unapoamini na kutenda mambo yahusuyo biashara yako kwa imani na mtazamo kuwa
biashara yako ipo sio tuu kwa sababu ya kupata faida ili wewe ujinufaishe bali
huko kupata faida ni sehemu tuu ya malipo yako ya kukufanya uihudumie biashara
yako ifikie kile ambacho kweli haswa ndio lengo lake.
Hivyo kwa
mtazamo wa kisomi ni kuwa pamoja na kwamba wewe unajiita bosi, kiukweli wewe ni
mtumishi tuu wa hiyo biashara.
Itazame
biashara yako kama kiumbe ambacho kimekwisha zaliwa, kinahitaji kuishi kwa
miaka mingi iwezekanavyo. Hata hivyo chukulia binadamu pia kama anaishi tuu ili
mradi kukuche, haipendezi. Ndivyo kwa biashara pia. Unahitaji kuikuza,
unahitaji kuifanya ionekane na yenywe ya muhimu. Unahitaji kuilinda dhidi ya
majanga, na pale inapoumwa (kukosa wateja, au changamoto nyingine za biashara)
wewe kama mzazi wake unatakiwa kuisaidia kurudi kwenye afya njema na pia
kuikinga isipate matatizo tena.
Hata hivyo
wapo pia wazazi wanaozaa watoto wakawatelekeza, wapo wazazi ambao wanazaa
watoto ili mradi tuu na wao waseme wana watoto , lakini mpango wa kuwafanya hao
watoto wawe kweli wenye kufanya mambo ya msingi kimaisha hawana. Watoto
wanaishia kuishi maisha magumu, wengine wanaishia kuuawa kwa wizi.
Hapa tatizo
ni mpango-toka mwanzo mzazi hakuainisha nini anataka kufanya kwa ajili ya mtoto
wake ( Utasema kila mzazi anamtakia mema mtoto wake, ni kweli, ila neno mema ni
neno pana sana. Na pia
kutamani sio kutenda). Wakati mtoto anakua, ni jukumu la mzazi kumchunguza
mtoto na kumuandalia mazingira ya kuwa mtu bora. Ndivyo kwenye biashara pia,
tumesema ichukulie biashara yako kama kiumbe.
Jiulize maswali haya:-
1. Je, ni
jambo gani haswa la msingi biashara yako inafanya hapa duniani :
Biashara zote
tunazosema zinaendeshwa kisomi ni kuwa zimejifafanua wazi kuwa zipo kutatua
tatizo fulani. Zimejifafanua vema ni kwa namna gani zitatatua tatizo hilo. Na
vipi zinataka kujulikana katika ulimwengu huu. Maelezo haya ya kusudio la
biashara na muelekeo wake hutajwa katika
kitu kinachoitwa MISSION na VISION.
Unakumbuka
nilitaja hapo mwanzo kuwa kupata faida sio lazima iwe ndio dalili ya kuendesha
biashara kisomi. Ni kweli, wengine wanapata faida kwa dhuluma, kwa hongo, na
hata kwa kukandamiza wengine. Kiukweli wengine hawana hata bidhaa kweli halisi
wanayozalisha na itakayokuwa endelevu. Ni swala tuu la muda kwamba ni kipindi
chao cha “kutesa” au ni kwa sababu ndio wamejikuta wapo kwenye mtandao
unaowafanya wawe hapo walipo.
Hii inatuleta
kwenye pointi ya pili:
2. Biashara ya kisomi ina mpango kuifanya biashara iwe
endelevu.
Mipango na
mikakati ya mara kwa mara inafanywa ili kuifanya biashara iweze kujiendesha,
iwe kukua na pia isiwe tegemezi kwa maamuzi yasiyo ya kitaalamu. Kufanya
biashara endelevu ni pamoja na kuhakikisha kuwa biashara ina akiba ya kutosha,
ina uongozi wenye kuelewa biashara inaendeshwaje, na kuthamini utaalamu.
Nakumbuka
tuliwahi kuanzisha biashara na jamaa kadhaa ilikuwa ni wasomi tupu toka UDSM na
kweli kwa simu za mwanzo tulipata fedha hata hivyo hatukuwa na mipango endelevu
na uongozi wenye kuheshimu biashara. Ilikuwa ili mradi tuu tupate hela tugawane
siku ziende. Najua bado zipo biashara nyingi za namna hii zipo ndogo vile vile
au zinakaribia kufa. Au la zinaleta presha tuu kwa wamiliki.
3. Biashara
inayoendeshwa kisomi imemuweka mteja kwanza:
Mteja ndio haswa bosi wa kweli
kwani yeyé anaweza kumwachisha kazi hata mmiliki wa biashara (Subiri biashara
yako ikose wateja uone kama hautofunga). Hivyo biashara ya kisomi ili ibaki
kuwa endelevu inabidi itumie muda wa kutosha kujifunza tabia, mahitaji na uwezo
wa wateja katika kununua bidhaa. Inahitaji pia kujenga mahusiano bora, na zaidi
sana kuwa na mbinu za kufikia wateja wapya zaidi na zaidi.
Biashara
inayoendeshwa kisomi inazingatia kuwa na bidhaa sahihi: Ndio ukweli ulivyo, kwamba ili wateja
waendelee kukuajiri inabidi uwe na kitu sahihi cha kutatua mahitaji yako. Hivyo
basi ni muhimu kuwa na bidhaa yenye kutimiza mahitaji ya wateja wako. Na
kama alivyowahi kusemaKumbuka maneno haya ya Seth Godin, gwiji wa marketing :
"Quality doesn't mean perfection. It means keeping the promise the customer wants you to keep. "
Yaani:
Ubora wa bidhaa hauna maana utengeneze kitu kisicho na mapungufu , bali ina maanisha kuwa utimize ahadi ambayo mteja anataka uitimize.
4. Biashara inayoendeshwa kisomi inazingatia kuwa na usimamizi
ulio imara:
Usimamizi imara hapa unaanza kwanza kwenye ujuzi wa bidhaa husika
inayozalishwa au kuuzwa, pia ujuzi wa mambo mengine ya msingi kama vile
usimamizi wa fedha, usimamizi wa wafanyakazi, mawasiliano sanifu, ujuzi wa masoko, uwezo wa kuweka mipango, kodi, na ujuzi wa kusoma
mazingira na mabadiliko katika jamii ili kuweza kuendana na mabadiliko. Sio
lazima mmiliki wa biashara ajue yote haya, ila anaweza kuajiri watu wenye ujuzi
wa mambo husika wamsaidie.
I like it. Thanks again
ReplyDeleteOkay
ReplyDeleteMungu azidi kukupa maisha marefu kwa elimu hii unayoipa jamii
ReplyDelete