FAHAMU JINSI YA KUANZA KUTIMIZA NDOTO YAKO HATA KAMA UNADHANI NI NGUMU


Kinachofanya watu wafanikiwe ukiacha bahati ni swala la kujituma katika wayafanyayo. Haitoshi tuu kuota na kutamani kuwa wa aina fulani, haitoshi tuu kuwa na mipango na mikakati isiyo na utekelezaji.

Wengi hupenda kuwa watu wa visingizio yaani kutoa sababu ya kwanini hawafanyi watakiwayo kufanya au kwanini hawajawa vile wanavyotamani kuwa. Mara nyingi sababu wazitoazo ni wazi kuwa hazitaji kwamba wao pia wanahusika na hali waliyonayo. Mara nyingi visingizio ni watu wengine kuwakwamisha, au mazingira.

Ukitaka mabadiliko siku zote fikiria kwamba sawa pamoja na yote unayoyaona kuwa ni magumu, je wewe kweli nini unaweza kufanya, hata kama ni kidogo.

Pengine tatizo ni namna ya tabia yako ilivyo, pengine ni majivuno yako na kujiona wa thamani zaidi au haufai kukabiliana na changamoto. Pengine ni kwakuwa haupo tayari kusamehe, au kuendana na watu fulani ili mambo yaende sawa. Pengine unahitaji ka uvumilivu kadogo tuu ili mambo yako yaende sawa.
Kanuni rahisi ya kukumbuka katika kuwajibika na kuepukana kuwa mtu wa sababu ni kuamini kuwa lengo lako ni la msingi zaidi kuliko hayo yanayokukwamisha. Anza sasa kuweka mbele ndoto yako na usikubali mtu au mazingira yakufanye urudi nyuma.

Usikubali watu-wasemayo au tabia zao ziwe kikwazo cha ndoto yako kwani hayo ni mawazo yao, kumbuka hata wewe una mawazo ambayo wengine hawawezi kuyabadilisha. Usikubali kuweka mtazamo wa mtu mwingine mbele au unayodhani anawaza juu yako mbele kuliko ndoto yako yenye thamani zaidi.

Kuhusu mazingira, kama huwezi kubadili mazingira uliyopo basi vumilia na thaminisha kuwa ni ndoto yako ni bora zaidi kuliko kuwa mnyonge wa mazingira. Ukifikira zaidi utaona mazingira hayo magumu yanakupa fursa.
Share:

2 comments:

  1. Maoni yangu. Ongeza font kidogo iwe kubwa kwa wwnye matatizo ya macho wanaweza kupata tabu.

    Asante sana

    ReplyDelete