KWA MUONGOZO HUU HATA WEWE WAWEZA ANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA


Unapotaka kujifunza kitu au mada husika ni vema ukaelewa kwanza maana ya kichwa cha habari, na mantiki ya kitu husika kuitwa hivyo kiitwavyo. 
Kuelewa huko kutakuwezesha kuelewa zaidi yale utakayosoma ndani ya mada husika, na hata mpangilio wa kitu husika.
Nikupe mfano: MCHANGANUO WA BIASHARA.
Hapa kuna maneno mawili -mchanganuo na neno Biashara.
Elewa kuwa kitu kilicho changanuliwa maana yake ni kuwa kimefafanuliwa kwa vipande vidogo vidogo ili kukupa uelewa wa jinsi kilivyo hivyo kilivyo kizima.
Neno biashara ni shughuli yeyote inayolenga kuleta faida.
Hivyo ukiunganisha maneno hayo mawili yaani Mchanganuo , na Biashara, unapata kujua kuwa basi Mchanganuo wa biashara itakuwa ni maelezo ya kina jinsi biashara biashara husika imeundwa.
--Kwa kufikiria hivyo haraka haraka tuu unajua basi mchanguo wa biashara ili kweli ukupatie hiyo picha kamili ya biashara - hivyo lazima tuifafanue biashara katika visehemu vyake vidogo vidogo kama vile, je biashara husika inahusu nini, nani ni wateja wa hiyo biashara, kwanini hao ni wateja wa hiyo biashara, ielezwe wazi bei za bidhaa husika, kiwango cha mauzo walau kiwa wiki, kwa mwezi, kwa mwaka, na hata miaka 3. 
Ielezwe wazi wazi mapato yatakuwa yapi katika tshs., kwa mwezi, mwaka n.k
Ielezwe vema gharama ni zipi, na ni kiasi gani katika tshs. Pia tujue wazi ni kwa mwezi, mwaka, n.k
Ielezwe usimamizi wa biashara utakuwa wa aina gani, nani atafanya shughuli zipi na atawajibika kwa nani.
Taarifa za fedha za mwezi, mwaka na miaka kadhaa kama 3 hivi zifafanue muonekane wa kifedha wa biashara husika.
Pia ielezwe changamoto zinazotegemewa kuikumba biashara na pia maandalizi yaliyopo kukabiliana na hizo changamoto.
--Si umeona? Ukisoma maelezo hayo yote yanakupa kweli picha nzima ya biashara lakini katika vipande vidogo vidogo. Kwa jinsi utakavyochambua unaondoa mashaka yoyote ya mtu kusema haielewi kitu kuhusu biashara husika. Mfano hauwezi tuu kusema unataraji kupata mapato kila mwezi laki 2, bila kuchambua hiyo laki mbili itapatikanaje.
Share:

0 comments:

Post a Comment