JIFUNZE KIINGEREZA SOMO LA 3: ADVANCED PRESENT CONTINOUS TENSE

Kaitka somo la leo tunajifunza mambo mengine ya msingi katika Present Continous tense.
Somo hili ni muendelezo wa somo lililopita. Kama haukusoma tafadhali bofya hapa kusoma.

VITENDO MAALUM VISIVYOTUMIA ING
Umejifunza kuwa ili kutunga sentensi katika present continous ni lazima vitendo viwe katika ING, mfano He is drinking, We are going to school, n.k
Hata hivyo kuna vitendo ambavyo hautakiwi kutumia ING. Mfano wa vitendo hivyo ni:
  • Love (Penda):  Ni makosa kusema I am loving you now. Sema  I love you.
  • Hear (Sikia):  Sio I am hearing you. Ila sema I HEAR you now.
  •  See (Ona):  Sio We are seeing them. Ila sema  We SEE them. ( Tunawaona)
  • Need (Hitaji): Sio We are needing it now. Ila sema We NEED it now. (Tunakihitaji sasa)
  • Want (Kutaka kitu). Sio She is wanting ugali. Ila sema She WANTS ugali. (Yeye anataka ugali)
  • Like (Kupenda). Sio I am liking it. Ila sema I LIKE it.
  • Know (Fahamu). Sio  She is knowing a lot. Ila sema She  KNOWS a lot . ( Yeye anafahamu mengi)
  • Remember (Kumbuka). Sio I am remembering now. Ila sema I REMEMBER now. (Ninakumbuka sasa)
  • Understand (elewa): Sio I am understanding you . Ila sema I UNDERSTAND you. (Ninakuelewa)

Hivyo kumbuka kuwa kwa vitendo hivi Love, Hear, See, Need , Want, Like, Know, Remember , na Undersand huwa tunatumia PRESENT SIMPLE TENSE hata kama matendo husika yanahusu PRESENT CONTIONUS TENSE.
Vitendo vingine vinavyofuata sheria hiyo hapo juu niliyoeleza ni want, cost, own, care, contain, owe, possess, seem, belong na exist, 

Katika somo litakalofuata utajifunza Zaidi kuhusu PRESENT SIMPLE TENSE.

VERB TO BE
Jinsi ya kuelezea namna watu au vitu vilivyo: ( TO BE), na ili kuelezea hali kwa mfano:-
Huyu ni mgonjwa
Yule ni mzima
Sisi tunafuraha
Unahitaji kujua namna ya kutumia Verb To (Yaani AM, IS na ARE) kwa wakati uliopo hali ya kuendelea.
Umeshasoma jinsi ya kutumia AM, IS na ARE ila kumbuka ulijifunza kutumia hizo AM, IS  na ARE pamoja na vitendo mfano ulijifunza kusema HE  IS READING (Anasoma), WE ARE NOT COMING (Sisi hatuji).
Ni vema ukajua utofauti wa IS, ARE, AM kama verb to be, na  wakati ambapo tunazitumia kuunganisha na vitendo. Umeona kuwa IS, ARE , AM zikitumika na vitendo lazima vitendo viwe na ING, mfano He IS reading.
Hata hivyo tunapozungumza IS , ARE , na AM kama Verb To, hapa hatuhusishi vitendo. Mfano
He is fine ( Yaani muda huu yeye yupo poa) Hapa mbele ya IS hakuna kitendo.
We are happy now. ( Muda huu, sisi tuna furaha). Hapa mbele ya ARE hakuna kitendo.

ACTIVE VOICE and PASSIVE VOICE:
Unapotunga sentensi una uchaguzi wa kuanza na mtendaji wa tendo kama vile

John anaandika barua.( John is writing a letter)- Hapa mtendaji ni John, na anachokitenda ni BARUA.
Mtindo huu wa kuanza na mtenda wa tukio , tunaita ACTIVE VOICE.

Hata hivyo unaweza pia kuamua kuanza na Mtendwa, mfano:
Barua inaandikwa na John ( A letter is being written by John).
Wao wanafundishwa na Issa( They are being taught by Issa).
Mtindo huu wa kuanza na mtendwa wa tukio , tunaita PASSIVE VOICE

Umegundua nini ?
Ni kwamba kama unaanza na mtendewa wa tendo basi ni lazima utumie neno BEING, halafu kitendo kibadilishwe kiwe katika mtindo tuuitao Past Participle. 
Mfano:
WRITE inakuwa WRITTEN,  
Teach inakuwa TAUGHT n.k. 

Kujua past participle za vitendo vingine Zaidi.  

Tafadhali BOFYA HAPA kudownload hapa orodha ya vitendo na past participle zake
Share:

3 comments: