Fans siku njema ya ijumaa.
Tafakari yetu leo inahusu FURAHA.
--Bila shaka furaha ndio lengo kuu la lolote ulifanyalo la kidunia na kiroho. Kwani ni wazi kuwa unaamini kuwa ukifanya vema utaenda kuishi ahera/mbinguni - ambako utakuwa mwenye furaha siku zote.
-- La msingi zaidi tunapotafakari kuhusu furaha tujiulize:-
1. Je, unatofautishaje furaha na burudani ?: Wakati mwingine unaweza kudhani kuwa burudani itakuletea furaha kumbe ni karaha.
2. Furaha ni swala la kiakili au kifikra zaidi kuliko lilivyo kifedha, mahali ulipo au nini kingine unacho. Mfano waweza dhani kuwa na mume au mke mzuri na mwenye fedha kutakufanya uishi kwa furaha, lakini umesahau wapo wa namna hiyo walioshia mmoja kumuua mwenzake! Unadhani fedha itakufanya ule bata na hivyo kuwa mwenye furaha, umesahau kuwa kuna mabilionea kama Adolf Merckle wa Ujerumani aliyeamua kujiua mwaka 2009 kisa eti familia yake ilianza kuingia kwenye madeni , au hukusikia habari ya Boris Berezovsky, bilionea wa Kirusi aliyekufa kwasababu ya huzuni baada ya kuona atakabiliwa na madeni (Hawa wote sio kwamba hela hawakuwa nazo bali hawakuridhika).
3. Na kama furaha ni muhimu kiasi hicho , je unafanya nini kuwa na furaha na kuilinda furaha yako ? Hakuna mtu anayeweza kuiondoa furaha yako ya kweli. Tunaamini ahera/mbinguni tutakuwa na furaha kwa kuwa huko hakutokuwa na vitu vitakavyotuharibia tafakari zetu. Tutakuwa wenye mawazo chanya, hakutokuwa na mazingira ambayo yanatufanya leo hii tujione wanyonge, au tuliopungukiwa.
--Jitahidi kuwa na mawazo chanya, jitahidi kujiamini na kupenda kujifunza mambo mengi ili uweze kuongoza vema hisia zako, mazingira yako n.k.
Kwa mfano hata kama mazingira ya kazi ni magumu, yasikufanye ujione ndio dunia haifai, bali tafuta kitu cha kukupa moyo katika magumu hayo unayopitia.
Hii pia ni hata kwa familia zetu kama maisha ni magumu bado twaweza kuwa wenye furaha na tusio kata tamaa.
0 comments:
Post a Comment