Jina lake halisi ni Curtis Jackson Jackson. 50cents anatajwa kuwa "Master Marketer" (Mtu wa kufanya shughuli za masoko mwenye uzoefu mkubwa) na Wall Street Journal. 50cents ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa dola za kimarekani 250, bado yupo kwenye muziki lakini sehemu kubwa ya mapato yake ni kutokana na shughuli nyingine nje ya muziki.
Kikubwa alichofanya 50cent ni kutumia umaarufu wake kujijenga kijasiriamali. Pia tofauti na wanamuziki wengine anajishughulisha yeye mwenyewe katika shughuli zake za ujasiriamali yeye akiwa ndiye msemaji mkuu wa shughuli zake.
50cent anasema kuwa mambo mengi tunayofanya ni maamuzi yetu mwenyewe, mfano anasema kuwa pamoja na kuuza madawa ya kulevya, bado hakuona kuvuta madawa kama uamuzi mzuri kwakuwa isingemsaidia. Uamuzi wake anasema ulikuwa uamuzi wa kibiashara zaidi na sio tuu jambo la kukataa kuvuta bangi.
Wasanii hususani wale walio maarufu bongo wanaweza kujifunza toka kwa 50cent
- Kutokutegemea tuu usanii wao, na wajitoe kweli kweli sio tuu kuanzisha biashara lakini pia waweze kujifunza kuendesha wao wenyewe kwa ufanisi.
- Na zaidi sana wasilizike na mafanikio na sifa toka kwa jamii, waamini kuwa wana nafasi kubwa ya kutumia umaarufu wao kujikwamua na kuwekeza na kwakufanya hivyo watatoa ajira kwa watu wengine.
Ujasiriamali wa 50cent upo wazi katika shughuli hizi:-
1. Uandishi wa vitabu: Kitabu cha The 50th Law , na kingine cha hivi karibuni Formula 50.
2. Alitengeneza raba za G-UNIT akishirikiana na Reebook. Hata hivyo kwa sasa aina hiyo ya raba inamilikiwa na Ecko.
3. Ana kampuni ya kutengeneza movie iitwayo Cheetah Vision.
4. Ni muigizaji filamu pia. Cheki filamu hii aliyowahi kuigiza inaitwa Self I Destruct.
5. Ana kampuni ya kutengeneza na kusambaza head phone ziitwazo SMS Audio.
6. Ana kampuni ya kutengeneza kinywaji cha kuongeza nguvu kiitwacho SK Energy.
7. Ana kampuni ya kuwafanyia "promo" mabondia, ijulikanayo kwa jina la SMS Promotions.
0 comments:
Post a Comment