Picha na Nairaland.com |
Hata hivyo gari hilo lililogunduliwa na Dokta Ezekiel Izuogu, wa huko Nigeria leo hii halipo sokoni baada ya kile anachodai mgunduzi huyo "fitina" na kutokupenda maendeleo kwa baadhi ya watu nchini kwake, kama alivyonukuliwa na imostateblog.
Kilichotokea ni kuwa uzalishaji wa magari kama hilo ambalo lilibuniwa mwaka 1997 na vifaa vyake kutengenezwa huko huko Nigeria, ulishindwa kuendelea kwakuwa majambazi wenye silaha walivamia kiwanda cha Dr. Izuogu tarehe 1 Machi 2006 na kuiba vifaa vyote muhimu vya uzalishaji wa gari hilo pamoja na vitabu vya jinsi ya kutengeneza gari hilo.
Wakati wizi huo unafanyika, Dr. Izuogu tayari alikuwa amekwisha pata "mchongo" wa kuruhusiwa kuanzisha kiwanda nchini Afrika Kusini cha kutengeneza magari hayo ya Izuogu -Z600.
Kwa mujibu wa Dr. Izuogu mwenyewe ambaye alitumia miaka mingi kubuni gari hilo ni kuwa wizi uliofanyika kiwanda chake ulivunja matumaini yote ya ndoto yake kukamilika.
Hata hivyo wapo watu huko Nigeria wanaomlaumu dokta huyo kwakuacha yeye mwenyewe wazo lake life. Wengine wanalaumu chuki za kimaendeleo miongoni mwa waAfrika wenyewe.
JE, wewe unasemaje ? Nani wa kulaumiwa ?Kwani gari hili kama uzalishaji wake ungefanikiwa basi lingeweza kuwa gari la bei nafuu zaidi Afrika.
0 comments:
Post a Comment