JIFUNZE KIINGEREZA SOMO LA 2 : TENSES

Katika somo hili utajifunza kuhusu nyakati (tenses) na tutaanza na wakati uliopo katika hali ya kuendelea (Present Continous Tense)
Katika kujifunza nyakati yoyote unatakiwa ukumbuke mambo haya makuu matatu:
  • Nyakati husika inatumikaje
  • Kanuni inayoongoza muundo wa nyakati husika
  • Namna ya kupangilia mionekano tofauti ya sentensi. 

(Kumbuka tulijifunza katika somo la kwanza kuhusu mionekano ya sentensi kama haukusoma tafadhali soma BOFYA HAPA)

1. Present Contious Tense inatumikaje:
Tense hii ina matumizi makuu mawili:-
A. Huwa tunatumia nyakati hii kuelezea matendo ambayo kweli kweli yanatenda kwa muda husika. Mfano:  You are Reading this article. ( Unasoma makala hii)
              We are studying English this month. (Tunasoma kiingereza mwezi huu)
Kumbuka present continuous sio lazima iwe wakati haswa wa sasa hivi, bali ni wakati uliopo na unaoendelea ndio maana twaweza sema “We are studying English this month” yaani bado tupo ndani ya huu mwezi , ingawaje pengine wakati tunataja hiyo sentensi, hatufanyi hilo tendo la kusoma, lakini tunaamini kabisa kuwa tendo la kusoma bado linaendelea kwakuwa mwezi haujaisha.
B. Pia Present Continous Tense hutumika kuelezea matukio ambayo yanakuja kutokea au hayotoweza kutokea ndani ya  muda si mrefu hapo baadae. kuyatenda wakati ujao. 
I am eating Ugali tomorrow afternoon. ( Ninakula ugali kesho mchana). Ingawaje hii kwa Kiswahili inaweza isiwe sahihi kusema ninakula ugali kesho, ila katika kiingereza inakubalika.
C. Huwa tunatumia nyakati hii kuelezea matendo ambayo hutokea kila mara au kitu ambacho kinakukera mara kwa mara. Hata hivyo matumizi ya Present continous tense katika hili ni lazima utumie neno ALWAYS ambalo lina maana "Daima"
Mfano: He is always coming later.  (Yeye daima huchelewa).

2. Kanuni inayoongoza muundo wa nyakati husika
Kuna kanuni kuu mbili za kuzingatia katika Present Continous tense nazo ni 
A. Hakikisha unatumia neno AM, IS au ARE kabla ya kutaja kitendo – ndio maana mifano ya sentensi hapo juu ilikuwa hivi:
 You are Reading this article. ( Unasoma makala hii)
              We are studying English this month. (Tunasoma kiingereza mwezi huu)
I am eating ugali tomorrow morning.
John is writing a letter. (John anaandika barua)
      Jinsi ya kutumia AM, IS na ARE
AM: Tumia AM kwa kiwakilishi I, yaani mimi. Mfano I am dancing. (Mimi ninacheza muziki).
IS : Tumia IS kwa viwakilishi He , She na IT, au kwa kitu au mtu mmoja mmoja. Mfano
She is eating (yeye anakula)
John is reading ( John anasoma)
ARE: Tumia ARE kwa viwakilishi hivi  We (Sisi), They (Wao) . Au kwa  watu au vitu vingi mfano:
We are eating (Sisi tunakula)
They are watching TV ( Wao wanaangalia TV)
John and Issa are playing soccer. ( John na Issa wanacheza soka)

B. Kanuni nyingine hakikisha vitendo vyote vinaishia na ING.
Mfano kitendo cha kucheza mpira ni PLAY ila ni lazima kiishie na neno ING hivyo kitakuwa PLAYING,
Kitendo kuangalia WATCH ni lazima kiishie na ING hivyo kitakuwa WATCHING.

3. Namna ya kupangilia mionekano tofauti ya sentensi
A. Muonekano wa kukubali:
Hakikisha maneno IS, ARE,AM yanafuata kiwakilishi au jina , na baada ya IS, ARE, AM ndio kifuate kitendo.
Hivyo tuna JINA/KIWAKILISHI +  IS/ARE/AM +KITENDO +..MANENO MENGINE KAMA YALIZMA
Mfano I am eating ugali
          We are talking
        She is drinking
B. Muonekano  wa kukanusha.
Ili kukanusha hakikisha unaweka tuu neno NO baada ya maneno IS, ARE, au AM kabla ya kutaja kitendo.
Hivyo itakuwa We are NOT eating
She is NOT drinking

C. Muonekano wa kuuliza swali
Hakikisha unaanza na maneno IS, ARE , AM, halafu ufuatie JINA au KIWAKILISHI, kisha malizia na kitendo.
Mfano:
Is she eating ? (Je, anakula ?)
Is she not eating ? (Je, hali ?)
Are we not coming ? ( Je, hatuji ?)

Am I not talking  ?( Je, mie sizungumzi ?)
Is John doing his work ? ( Je John anafanya kazi yake?)
---Tutaendelea tena IJUMAA ya wiki hii. Kama una swali usisite kuniuliza, nicheki Facebook kwa kubofya hapa. 
Share:

3 comments: