Ndiyo mara nyingi watu wamekuwa wakilalamika kuwa kuna watu wanapost vitu kwa akaunti zao za FB bila ruhusa.
La msingi kuelewa ni kuwa kwa kiwango kikubwa chanzo cha hao watu kupost kwa akaunti yako kama vile ni wewe ndiye unayepost, ni kwakuwa wewe mwenyewe umeruhusu kufanya hivyo.
Haijalishi kama umetoa ruhusa kwa kukusudia au kutokukusudia , lakini ni wewe mwenye akaunti ya FB ndio chanzo cha matatizo hayo.
Kivipi ?
1. Unapo comment kwa
websites au blog
Mfano wa sehemu ya kuacha comment. Picha na Techcrunch.com |
Kuna websites na blogs nyingi hutumia kitu kiitwa Facebook
plugin, yaani mkusanyiko wa codes fulani ambazo pamoja na kuruhusu kupost
katika website au blog husika, pia huonyesha ulicho comment kwa akaunti yako ya
Facebook.
2. Unaporuhusu apps
kutumia akaunti yako
Kuna namna mbili za kuruhusu apps kutumia akaunti yako:
A. Kwanza: Ni wewe
mwenyewe unakuwa unajua kabisa kuwa unaruhusu app husika kufanya hivyo. Mfano
kama umetembelea website ya yahoo au bbc na ukakubali kujiandikisha kwa
application (app) yao, basi utapata maelekezo kuwa unatakiwa uruhusu app husika
itumie taarifa za akaunti yako, na pia itakueleza kuwa kuna wakati inaweza
ikapost vitu kwa niaba yako.
Hivyo kama hautaki app ifanye hivyo hakikisha unaacha
kukubali hayo maelezo. Hivyo hautoweza kuitumia hiyo app.
Usiposoma makini vitu kama hivi waweza kukuta unaambiwa kabisa kuwa app itakuwa ikipost kwa niaba yako, ila wewe unakubali tuu. |
B. Pili: Waweza kuruhusu app bila wewe mwenyewe kujijua.
Hii inaweza kutokea pale ambapo una
click tuu link usiyoijua na kujikuta unapokea maelekezo tofauti tofauti.
Maelekezo mengine yanaweza kukuchanganya na kwakuwa waweza kuwa na haraka
ukajikuta usisome kwa umakini maelekezo unayopokea hivyo kubofya sehemu ambayo
itapelekea kutoa ruhusa kwa apps kuitumia akaunti yako. Angalia mfano pichani mwanzoni kabisa ambapo post inakudanganya kuhusu mwanamieleka wa WWE na wewe kwakuwa unataka kufuatilia habari utabofya link. Kubofya kwa link kama hizo kwaweza kukupelekea kuruhusu watu wengine watumie akaunti yako.
3. Unapokuwa umeibiwa akaunti yako bila kujijua
Kuna namna mbalimbali za kuibiwa akaunti yako ya FB bila
kujijua:-
A. Kwa ku-sign in
akaunti yako ya FB katika website feki ya FB: Kuna watu wanaweza kutengeneza websites
zinazoonekana sawa sawa kabisa na FB hata hivyo kiukweli sio, katika lugha ya
kitaalamu mtindo huu unaitwa phishing. Hivyo wakishakuingiza mjini na kupata password
na jina lako unalotumia FB, wanaweza kuitumia akaunti yako kwa namna yoyote
wanayopenda wao.
Kwa kuruhusu
extension maalum zinazohusu Facebook: Fahamu maana ya neno extension ni
kuwa ni program maalum unayoingiza katika kompyuta yako ili kusaidia web
browser kama Mozila Firefox, Internet Explorer au Google Chrome ili kuboresha
ufanyaji kazi wa browser husika au kukupa uwanja mpana Zaidi wa matumizi ya
website fulani utakayoitembelea. Mfano zipo Facebook extension iitwayo Facebook Chart Alert inakuwezesha kupata notification kuwa rafiki yako ame sign in FB pale
mmoja wa rafiki yako afanyavyo hivyo. OK, natumaini umeelewa maana ya
EXTENSION.
Hitimisho :
Je, dawa ni nini ?
Elewa kuwa
una jukumu la kuwa makini wewe mwenyewe ili usikumbwe na majanga hayo hapo juu.
Mfano hakikisha hau click links usizozijua. Hakikisha unasoma maelekezo vema ya
chochote kinachojitokeza wakati unatumia FB kujua kama kinakutaka ukiruhusu
kitumie akaunti yako.
Pia
hakikisha unakuwa makini na website ya Facebook unayofungua kwani pengine ni
feki. Hata unapodownload apps kwa ajili ya matumizi ya FB kama vile Facebook
Messenger hakikisha umeitoa sehemu kweli ya kuaminika kama vile Google Store.
Kuhusu kuondoa APPS usizozihitaji
Ingia kwa settings za akaunti yako sehemu ya APPS (Cheki kushoto kwa kompyuta yako) kisha fuata maelekezo katika ukurasa huo wa APP kwa ku remove app husika.
0 comments:
Post a Comment