FAHAMU NENO NIGGER NA MENGINE YALIYOPIGWA MARUFUKU

Ndio, umesikia mara nyingi neno nigger likitumika kuelezea mtu mweusi. Hata hivyo nchini MAREKANI, neno hilo limepigwa marufuku kwakuwa linadhalilisha au kukashifu watu weusi.

Na kama habari hiyo haitoshi yafuatayo ni maneno ambayo yanapendekezwa yasitumike huko Marekani :-
Selfie : ambalo maana yake ni kujipiga picha wewe mwenyewe
Hashtag: ambalo linamaanisha ile alama ya # inayotumika kwenye mitandao mingi ya kijamii
YOLO: Kifupi cha sentensi You Only Live Once (Unaishi mara moja tuu)
Twerk:  Aina fulani ya kucheza muziki

Google wao walikwishatoa ondoa baadhi ya maneno katika kamusi yao ya Android, maneno ambayo yameondolewa na Google katika kamusi yao ni pamoja na:
Geek
Sunni
Iftar
Condom
Sex
Yaani kinachotokea hapa kwa Google ni kuwa ukiwa mtumiaji wa simu au kifaa kingine kinachotumia Android, basi kama utaenda kuandika maneno mara nyingi kamusi ya Google huwa inakamilisha maneno kwa ajili yako hivyo hautakiwa kutype neno zima. Hata hivyo kwa maneno ambayo yamepigwa marufuku na Google itakupasa kukamilisha herufi zote wewe mwenyewe kwa kuwa kifaa chako hakitambui neno husika.

Je, na sisi nchini mwetu Tanzania kama kupiga marufuku maneno, wewe ungependekeza yapi yasitumike ?


Share:

0 comments:

Post a Comment