KWANINI KILA JAMBO LINA FAIDA ILA WEWE TUU HUIONI


Kuna mtu ameniuliza swali mbona Mbuke Times haina matangazo ya biashara sasa ninapataje faida ? Si ni bora niache kwa kuwa ni kama napoteza muda wangu na nguvu zangu.
Akanikumbusha nizungumze kasumba ambayo mara nyingi watu wengi wanayo ambayo ni kuangalia faida ya kifedha, tena hela inayoingia wakati huo huo au ndani ya muda mfupi ujao.



Yawezekana hauna tabia ya kufikiria namna ya kutengeneza faida ya baadae, inawezekana mtazamo wako ni wa aina moja tuu kuhusu unavyoweza kunufaika na jambo fulani.



Itazame faida kwa namna hii:-
1. Inawezekana fadia kweli ya hela ikaingia baadae sio lazima sasa.
2. Inawezekana ukapata fedha kwa njia tofauti na hiyo unayodhani lakini hiyo njia nyingine ni kwa sababu ya hilo jambo ambalo unadhani halina faida.
3. Faida sio lazima iwe fedha, kwan hata kukutana na watu wengine, wewe mwenyewe kujifunza mambo, kupata uzoefu wa shughuli husika, na pengine katka kufanya hivyo ukachochewa kujishughulisha na jambo lingine zaidi. Mfano kuandika kwangu blog , kumenichochea kusoma IT kwa nguvu zote. Hii ni faida ambayo siwezi kuipima kifedha.
--Shughuli za NGOs na kujitolea zimenipa fikra pana za kimaisha kwani unapofanya kazi na watu wasiojiweza kimwili na kifedha unapata kujua namna maisha yalivyo kwa upana zaidi.


HIVYO ACHA KUAHIRISHA KUFANYA MAMBO YA MSINGI , eti kwa sababu HAUONI FAIDA. Mtu mwingine hata kujisomea tuu atasema haoni faida, kwani anasema anasubiri apate kusoma ambako kutampata CHETI. Yaani kwake KUJIELIMISHA kusiko na cheti huko HAKUNA FAIDA.
Share:

0 comments:

Post a Comment