VERB TO BE
Jinsi ya kuelezea namna watu au vitu
vilivyo: ( TO BE), na ili kuelezea hali kwa mfano:-
Huyu huwa mgonjwa daima
Yule yupo makini kila siku
Sisi ni watu wa
furaha siku zote.
Huwa tunatumia AM, IS na ARE) kwa simple present tense.
Umeshasoma jinsi ya kutumia AM, IS na
ARE ila kumbuka ulijifunza kutumia hizo AM, IS na ARE pamoja na vitendo
mfano ulijifunza kusema HE IS READING (Anasoma), WE ARE NOT COMING (Sisi
hatuji).
Ni vema ukajua utofauti wa IS, ARE,
AM kama verb to be, na wakati ambapo tunazitumia kuunganisha na vitendo.
Umeona kuwa IS, ARE , AM zikitumika na vitendo lazima vitendo viwe na ING,
mfano He IS reading.
Hata hivyo tunapozungumza IS , ARE ,
na AM kama Verb To katika simper present tense, hapa hatuhusishi vitendo. Mfano
He is always careful. ( Daima yupo
makini)
We are always happy people. (Sisi ni watu wa furaha siku zote.)
Daima nipo mwenye huzuni. ( I am always
sad)
ACTIVE VOICE and PASSIVE VOICE:
Unapotunga
sentensi una uchaguzi wa kuanza na mtendaji wa tendo kama vile
John huandika barua.( John is writes letters)-
Hapa mtendaji ni John, na anachokitenda ni BARUA.
Mtindo huu wa
kuanza na mtenda wa tukio , tunaita ACTIVE VOICE.
Hata hivyo
unaweza pia kuamua kuanza na Mtendwa, mfano:
Barua huandikwa na John ( A letter is
written by John).
Wao hufundishwa na Issa( They are taught
by Issa).
Mie huitwa John. ( I am called John)
Mtindo huu wa kuanza na mtendwa wa
tukio , tunaita PASSIVE VOICE
Umegundua nini ?
Ni
kwamba kama unaanza na mtendewa wa tendo basi ni lazima utumie neno AM, IS au
ARE, halafu kitendo kibadilishwe kiwe katika mtindo tuuitao Past
Participle.
Mfano:
WRITE
inakuwa WRITTEN,
Teach
inakuwa TAUGHT n.k.
Call inakuwa CALLED.
0 comments:
Post a Comment