FAHAMU JINSI YA KUTAMBUA BAHATI


Tafakari yetu leo inahusu BAHATI
Ni kweli kuwa kuna kufanya bidii ili kufanikiwa, hata hivyo sio kila mafanikio yako basi ni kwa sababu ya juhudi zako. Basi tuseme yale ambayo yametokea kwa maisha yako bila wewe kuweka mipango au juhudi, basi hiyo ni bahati.
Wakati mwingne waweza kweli kuweka mipango na juhudi lakini ukapata matokeo ambayo ni zaidi ya hizo juhudi au mipango yako.Hiyo nayo ni bahati.
Kuna mambo mengine yapo wazi kabisa, mfano kuwa mzuri wa sura au umbo, kuwa wa kabila fulani, nchi fulani , wa mkoa fulani, na hata kuzaliwa katika familia fulani yote zote hizo ni bahati.

Mengine ya kukumbuka ya msingi kuhusu bahati ni kuwa:-
1. Ukitambua uwepo wa bahati mbalimbali ulizonazo utakuwa mnyenyekevu (usiye na makuu) na utaheshimu na kuthamini wengine ambao wana hali ya chini kwa kujilinganisha nao.
2. Bahati nyingine zinajitokeza kwa sababu ya juhudi binafsi na mipango pia. Mfano kwa juhudi zako za kufanya kazi vema, unapata bahati ya kukutana na bosi au wateja ambao wanakupatia dili kubwa zaidi ya kukutoa kimaisha. Nasema bahati kwakuwa sio kila mtu mwenye kufanya kazi kwa bidii na uaminifu atapata watu wa kumpa dili kubwa kubwa.
3. Kuna nyakati ili bahati ilete maana katika maisha yako ni lazima uwe umejiandaa kuitumia bahati husika, na hata ikiwepo ni lazima ufanye kazi kuilinda. Ndio maana wapo watoto wa matajiri wanakuja kuishi maisha ya kifukara, wapo waliobahatika kuwa watu maarufu ila wameshindwa kuutumia umaarufu wao kujiletea maendeleo. Wapo baadhi waliobahatika kuichezea timu ya taifa ungedhani pengine wangejibidiisha ili waonekane kimataifa, ila wameridhika na klabu zao.
Share:

0 comments:

Post a Comment