Kama unataka kuwa “up to date” na taarifa mbalimbali ziwe ni
makala toka website mbalimbali au habari za matukio mbalimbali, basi twitter,
ndio njia maarufu sana katika kukufanikisha katika hilo. Makala hii inakupa
maelezo ya jinsi ya kuanza kuitumia twitter, na pia kama umeanza kutumia basi
inakupa mwanga zaidi wa mambo ya msingi kufahamu ili kuboresha matumizi ya
twitter.
Twitter ni mtandao unaokuwezesha kuandika ujumbe mfupi wa
maneno usiozidi maneno 140 na ku ‘share’ . Ujumbe huo wa maneno 140, ndio
huitwa ‘tweet’, na kitendo cha kuandika
na kurusha hewani ‘tweet’ yako ndio huitwa “ku tweet”.
Unaweza pia ‘kushare’ tweets za watu wengine, kitendo cha
kushare tweets za watu wengine huitwa “ku retweet”.
Unaweza pia kutuma ujumbe kwa mtu binafsi aliyejiunga na
tweeter, endapo umejiunga nae katika mawasiliano yenu ya tweeter.
Je unajiunga vipi na
twitter
Ili kujiunga na twitter, kwanza inakupasa uwe na anuani ya
barua pepe (email address), kisha ingia www.twitter.com na utaona sehemu ya kujisajili (sign up). Katika
kujisajili kwanza utatakiwa kuandika Jina lako, na pia utatakiwa kuandika barua
pepe yako, na uandike password utakayokuwa ukiitumia kufungua hiyo akaunti yako
ya twitter. Ukishamaliza kufanya hivyo, bofya Sign Up for twitter, na utakutana
na ukurusa mwingine ambapo utakuwezesha kuchagua aina la jina utakalotumia
katika Twitter. Angalia sehemu imeandikwa “Choose your user name”.
Jina lako la twitter huitwa “handle”, hivyo mtu anaweza
kuambia “Niambie twitter handle yako”
Marafiki waliokualika au kukujumisha wewe kama rafiki yao katika twitter wanaitwa “followers”, na wale
unaowajumuisha wewe wanaitwa “following”. Mara kwa mara utapokea kutoka twitter
wenyewe mapendekezo ya akina nani uwajumuishe kama “following” wako, hata
hivyo, wewe mwenyewe pia unaweza kutafuta kwa sehemu ya search katika twitter
majina ya watu au habari unazotaka kufuatilia, kisha ukawajumuisha watu kama “following”
wako kwa kubofya sehemu ya “follow”
Je unapost vipi
‘status’:
Kushoto mwa ukurasa wako wa twitter kuna sehemu imeandikwa “
Compose new tweet”. Hapo ndipo unapoandika status yako na kisha kubofya “ TWEET”.
Utaona pia alama ya picha, basi bofya hapo kama unataka kupost picha.
Matumizi ya alama ya #
Kwa usahihi, alama ya # hutumika kuifanya status iingie
katika kundi maalum la aina ya status. Mfano kama utaweka #Majanga, basi
unailazimisha status yako iingizwe katika kundi la status zinazotumia hiyo
alama ya Majanga. Hii ina maana kuwa kama kuna watu wengine wametumia hiyo
alama ya #Majanga, basi nyote status zenu zitaorodheshwa huko.
Picha ya Profile yako
Kama ilivyo katika Facebook, unaweza pia kuweka picha mbili
kwa profile yako, ili kufanya hivyo nenda sehemu ya kuedit profile yako, (
Kulia juu mwa akaunti yako kisha bofya edit profile). Utakuta sehemu ya kuweka
Photo, na sehemu ya kuweka picha ya Header.
Kuunganisha akaunti
yako ya twitter na Facebook
Ndio, unaweza kuamuru twitter iwe inaonyesha tweets zako
kwenye akaunti yako ya Facebook. Ili kufanikiwa katika hilo, unatakiwa kuingia
sehemu ya Edit Profile, kisha angalia sehemu imeandikwa Connect to Facebook.
Bofya hapo kisha ufuate maelekezo utakayoambiwa.
Twitter katika simu
yako
Ndio unaweza kuitumia twitter kwa urahisi ukiwa ume download
na ku install program maalum kwa simu za mkononi. Ukiwa kwa simu yako, nenda
google.com, kisha waweza andika Download twitter for (android) kama simu yako
inatumia system za android. Kama ni Nokia, basi andika Download twitter for
Nokia. Kisha chagua chaguo la kwanza linalokupeleka kwenye ukurasa wa
kudownload hiyo program, ukiisha install, utaweza tumia vema twitter katika simu
yako.
Hata hivyo, hata kama hauna program ya twitter, unaweza
tumia twitter, kwa kuandika anuani ya twitter kwenye sehemu ya kuandika anuani
za website yaani www.twitter.com, kisha
fuata maelekezo kama unataka ku sign in, au ku sign up.
asante
ReplyDeleteMe Twitter yangu nikitaka kuingia inaniambia ,,I'm robot??nashindwa kuelewa why msaada pleas
ReplyDelete