Kwa bahati mbaya Google haitoi majibu ya swali hapo juu- yaani ni blog zipi za kibongo ambazo zinaingiza fedha zaidi, au ni bloggers gani wa kibongo wanaingiza fedha zaidi. Hata ukiuliza hilo swali hapo juu kwa kiingereza bado hautopata jibu.
Sina uhakika kama kuna mtu mwenye takwimu au taarifa za 'ranking' za namna hii kwa nchi yetu ya Tanzania. Kama kuna mwenye taarifa hizi anaweza kutupia maelezo au link hapo chini sehemu ya kutoa maoni.
Picha ya makala hii hapo chini inaonyesha bloggers 10 wenye kuingiza fedha zaidi huko India. Link, hii hapa inaonyesha blogs 50 zinazoingiza fedha zaidi huko nje ya Tanzania.
Hata hivyo, lengo la makala hii sio kutafuta majina ya akina nani hasa wanaingiza fedha nyingi bali kupitia makala hii nataka kuibua tafakari ya jinsi wenzetu wa nchi mbalimbali wanavyoweza kuingiza fedha nyingi kupitia blogs.
Yafuatayo ni mambo ya msingi unayoweza kuona kutoka nchi za wenzetu:
- Karibu blogu zote zinazoongoza kwa kuingiza fedha zinaandika mambo ya kimaendeleo hususani teknolojia
- Karibu blogu zote zinazoongoza kwa kingiza fedha zinaongozwa kitaalamu, na kwamba hata wamiliki wake wana upeo mkubwa wa mambo wanayoyaandika na pia uwezo mkubwa wa kusimamia blogu zao hata ikibidi kuandika 'codes'
- Hakuna blogu zilizoshika nafasi katika kumi bora kwa kuandika habari za udaku, na kuweka picha za ngono.
- Karibu blogu zote zinazoongoza kwa kuingiza fedha zimejikita kwa habari zenye kulenga aina fulani maalum ya wasomaji.
- Karibu blogu zote zinazoongoza kwa kuingiza fedha zina mwonekano mzuri sana , na kwamba matangazo hayachukui nafasi ya kwanza katika kuonekana. Msisitizo umewekwa kwenye kuonyesha kwa haraka makala za blogu husika.
- Karibu blogu zote zinazoongoza kwa kuingiza fedha zimejikita katika kuhakikisha 'search engine' zinazitambua kwa haraka na hivyo unapotafuta taarifa fulani mfano katika Google, majibu yako yatajumuisha makala toka blogu hizo, endapo unachotafuta kimeandikwa pia katika blogu husika. Hii inaitwa SEO ( Search Engine Optimization)
- Karibu blogu zote zinaoongoza kwa kuingiza fedha, zimejikita katika kuleta upekee, iwe kwa aina ya makala wanazoandika, au hata muonekano wa nje ya blogu husika.
ASANTE KWA UJUMBE MZURI HASA KWETU BLOGGERS.
ReplyDelete