Ni muhimu kuwa na utamaduni wa kuheshimu ndoto zetu hata kama tunadhani kuwa ni ndoto
ndogo kama vile ndoto ya kutembelea mkoa fulani, ndoto ya kutembelea nchi
fulani, ndoto ya kumiliki aina fulani ya mali, n.k. Hata hivyo, kuweza
kuheshimu ndoto zetu na kuzitimiza, kunahitaji nidhamu ya ziada, ingawa wapo
wanaozifikia ndoto zao kwa bahati.
Wengi husema wanataka kutimiza ndoto zao, hata
hivyo ni wachache hufanikiwa kutimiza ndoto zao. Kwa kuwa binadamu tuna ndoto
tofauti tofauti, ni ngumu kuwa na kanuni moja ya jinsi ya kufikia ndoto zetu,
hata hivyo uzoefu unaonyesha mambo kadhaa ambayo watu wengi waliofikia ndoto
zao wamefanya. Mambo haya ndio tunayojadili katika makala hii:-
1. Ota ndoto kwa usahihi: Kuota ndoto ya mabadiliko ya maisha yako, sio
tuu kuwaza au kutamani kufikia hali fulani, bali kuota kwa usahihi ni
kutengeneza picha kichwani ya hali unayotaka kufikia, au mambo unayotaka kuyapata.
Na zaidi sana, itengeneze picha ya hali unayotaka kufikiaau mambo unayotaka
kufikia katika mawazo yako kiasi kwamba ufikie hatua ‘unahisia za kuwa tayari
umefikia hali unayotaka au umeyapata hayo unayoyaota. Ikiwezekana weka katika
maandishi ndoto zako ili iwe rahisi kuzikumbuka mara kwa mara.
2. Tafakari kwa umakini: Ukishaipata kwa uhakika ndoto yako au ndoto zako, endelea kutafakari ili kutambua kwa undani ili kutambua mambo ya msingi kuhusu ndoto yako kama vile:-
2. Tafakari kwa umakini: Ukishaipata kwa uhakika ndoto yako au ndoto zako, endelea kutafakari ili kutambua kwa undani ili kutambua mambo ya msingi kuhusu ndoto yako kama vile:-
- Mambo gani utatakiwa kufanya (Mfano kiwango cha elimu, kujua lugha za kigeni, kupata uzoefu fulani, n.k)
- Aina ya mazingira yanahitajika ili kufikia ndoto hiyo (Mfano: Kupata washauri, Kujenga mtandao wa aina fulani ya watu n.k)
- Kiasi gani cha juhudi au bidii inabidi uwe nayo ili kufikikia ndoto huto zako. (Mfano: Mazoezi ya kila siku, kujaribu biashara mbalimbali, n.k)
- Aina gani ya msaada unahitajika (Mfano: Kama unahitaji fedha, unahitaji mtu wa kufundisha mambo fulani)
3. Weka mkakati: Mikakati ni yale yote unayoweza kufanya ili kufikia ndoto
zako. Kupitia tafakari uliyoifanya kama ilivyoelezwa hapo juu, utaweza kupanga
mbinu na namna ya kuzitekeleza mbinu za kufikia ndoto yako.
4. Amini na uwe mvumilivu: Tambua kuwa baadhi ya ndoto huchukua muda
kutimia. Na pia sio juhudi zote utakazofanya zinaweza kufanikiwa. Hivyo
unahitaji kuwa na uvumilivu na imani kubwa katika ndoto zako. Usichoke pia kuchunguza mara kwa mara mikakati
yako ili kuiboresha.
5. Fanya unachotakiwa kufanya kwa bidii na
maarifa: Kuwa na ndoto pekee hakufanyi
ndoto hizo kutimia. Unahitaji mikakati. Na zaidi sana unahitaji kufanyia kazi
mikakati yako. Kumbuka kuwa ingawaje kuna swala la watu kufikia ndoto zao kwa
bahati, tambua kuwa bahati ikikufikia wakati ambapo hauna uwezo au mazingira
uliyonayo hayakuruhusu kuitumia bahati husika, basi bahati hiyo haitokuwa na
maana kwako.
Hitimisho: Maelezo hapo juu yanahitaji tafakari ya umakini, na utilie
mkazo kila hatua. Anza kwa kuandika mambo unayodhani ndio ndoto zako. Usisahau
kutembelea mara kwa mara orodha yako ya ndoto, tafakari ni ndoto zipi umefikia
, na zile usizofikia tafakari jinsi ya kuzifikia. Nakutakia kila la kheri
katika kufikia ndoto zako, najua ni furaha sana kufikia ndoto, hata kaka ni
ndoto ‘ndogo’.
impressed
ReplyDeleteimpressed
ReplyDelete