Sikia hii kali kutoka kwa Bwana Mushi
mwanzilishi wa NIPENI DILI MASELA ambaye alipata kusikia mazungumzo kati
ya mzazi na kijana wake ambapo mazungumzo yalikuwa hivi:
Mzazi: Ukimaliza lasaba una mpango gani? Mtoto: "Nimepanga kuanzisha blogu"
Kichekesho hapo juu kinatukumbusha namna ambavyo suala
la blogging limeonekana kama aina fulani
ya biashara ambayo wengi wetu tungependa kuifanya. Na hata wengine kuamini kuwa
wanaweza kujiajiri kupitia biashara ya blogging.
Nimekuwa kwenye fani hii ya blogging kwa mwaka wa tatu sasa,
na pia nimekuwa nikijifunza kupitia kwa bloggers mbalimbali, na kusoma makala
za kitaalamu kuhusu fani hii inayokuwa kwa kasi sio tuu Tanzania, bali duniani
kwa ujumla. Yafuatayo ni mambo ya msingi
unayoweza kuchunguza ili kujua kama blogging itakuwa na faida kwako au la:-
1. Gharama
za kumiliki na kuendesha blog
Ingawa
ni kweli kuwa ni bure kabisa kuandikisha na kuifanya blog yako irushwe hewani
iwe kwa wordpress.com au blogger.com,
kumbuka kuna gharama nyingine nyingi kama kweli unataka blogu yako iwe na ubora
wa ushindani katika soko. Gharama hizo ni:-
- Gharama za fedha : Inapendeza pale unapokuwa na anuani maalum ya blog yako yaani badala ya kuwa na www.blogyako.blogspot.com, unakuwa na www.blogyako.com. Kupata anuani maalum (domain) itakubidi utumie fedha.Pia badala ya ku host na blogger au wordpress unaweza amua kuhamishia blog yako kwa taasisi zenye ku host kwa malipo. Gharama nyingi ni malipo ya kutengeza vizuri muonekano wa blog yako, gharama za usafiri kufuatilia habari, gharama za kuwepo mtandaoni – internet bundles, gharama za simu na pengine chakula unapokuwa unahangaikia kupata taarifa za kuweka kwa blogu yako.
- Gharama zisizo za fedha: Kuna gharama nyingine kama vile muda unaopoteza kushughulikia makala za blogu yako na kutafuta wasomaji. Pia gharama za usumbufu wa kiakili pale unapojikuta ukikata tamaa kwakuwa blogu yako haiendi vizuri, au unapopata upinzani usio wa maana toka kwa watu mbalimbali, hususani bloggers wenzako.
2. Mapato
yatokanayo na blogu
- Mapato ya moja kwa moja: Chanzo kikuu cha mapato kwa blogu ni matangazo. Unaweza kuwalipisha watu binafsi, makampuni, serikali na hata asasi mbalimbali zinazotaka kuweka matangazo kwa blogu yako. Chanzo kingine cha mapato ya matangazo ni kupitia huduma ya Google Adsense, ambapo blogu yako ikikidhi masharti ya Google Adsense , basi utaanza kuona matangazo yakiwekwa kwenye blogu yako, baada ya wewe kuwa ume omba huduma hiyo iwekwe kwa blogu yako. Google itakulipa commission kwa matangazo wanayoweka.
- Mapato mengineyo: Kuna nyakati blogu inaweza kukuingizia mapato kupitia ubunifu wako wa kuitumia kujenga mapato sehemu nyingine. Mfano blogu yako inaweza kukufanya ukajenga mtandao mkubwa wa ‘watu muhimu’. Hii itakurahisishia dili nyingine utakazotaka kufanya hapo baadae. Hata hivyo kujenga mtandao imara ni kazi kubwa. Soma hapa JINSI YA KUJENGA MTANDAO WENYE MANUFAA. Ukiwa na bidii katika blogu yako utalazimika kujifunza mambo mengi mapya,ya kiteknolojia, uandishi makini, marketing na hata namna ya kujenga mahusiano bora na watu wengine. Hizi ni faida kubwa sana kwa maisha yako.
3. Vifaa
vya kazi: Ili kufanya kazi zako za blogging kwa ufanisi unahitaji kuwa na
kompyuta, hususani laptop ili uwe na uhuru wa kufanya kazi mahali popote.
Kumbuka pia unaweza kutumia smartphones kuandaa na kurusha hewani makala zako.
Unahitaji kuwa na modem au sehemu yoyote ya uhakika ya kupata huduma ya
internet.
4. Kazi
za blogger
- Kuandaa makala
- Kutafuta habari
- Kupiga picha
- Kupost
- Kutafuta wasomaji
- Kutafuta wanunuaji wa nafasi za matangazo
- Kuendelea kujifunza mabadiliko mapya
- Kuweka Malengo na kusimamia ukuaji wa blog
hembu nisaidie hapo kwenye kutengeneza muundo wa blog au kutengeneza web yangu mwenyewe..nilazima ulipie au nilazima uwe na account benk?..namiliki blog nataka kuiboresha zaidi.... nijibu kwa email.yangu ..
ReplyDeleteraihopson@gmail.com
Mimi naweza kukusaidia kuboresha ikawa kama hii yangu
Deletebonnyupdates.blogspot.com
Whatsapp 0758794379
Pamoja kaka
ReplyDeleteAhsante kaka
DeleteUbarikiwe ndugu
ReplyDeleteAhsante kaka
DeleteNimejifunza kitu kipya nitakutafuteni mnifungulie Blog yangu
ReplyDeleteMimi ninayo blog ya worldpress naitaji kujua taratibu za kufanya kazi na makampuni tafadhali nisaidie
ReplyDelete