KUJIAMINI KWA USAHIHI KUPO HIVI..


Tafakari yetu leo inahusu mfano huu:- 
Umeenda hotelini na rafiki zako, mkaagiza vyakula kila mmoja anachopenda. Wewe ukaagiza kile haswa ukipendacho. Baada ya msosi katika mazungumzo mmoja wa rafiki yako akauliza ulijisikiaje wakati unakula chakula husika. Ukasema -ilikuwa bomba tuu. 
Rafiki zako wote wakacheka kusikia hivyo. Kichekecho cha kusanifu na wakasema wazi wazi kuwa wanadhani ulionekana mshamba kwa msosi uliokula. Wao wanafikiri ungetakiwa kula msosi wa 'kizungu zaidi' sio ule wa kawaida wa home kama ulioagiza. 
Wewe kusikia hivyo ukajisikia vibaya, ukajiona kweli umekuwa mshamba, ukajiona umeshuka thamani, ukapatwa na hasira juu yako kwa maamuzi mabaya. Hasira zikahamia kwa rafiki zako, ukawachukia kwa kukuona mshamba.
Hapo tunasema kuna tatizo la SELF ESTEEM. Yaani kuna tatizo la wewe kutojiamini, kutojithamini na kuthamini maamuzi yako. Hivyo kuweka mbele mtazamo wa wengine dhidi yako kuliko wewe uonavyo mambo na maamuzi juu yako mwenyewe.
Kumbuka ni wewe unayependa msosi uliokula iweje maoni ya wengine yakufanye uone uamuzi wako haukuwa sahihi ? Je, kweli wamebadili utamu wa msosi ?
--Unahitaji kujiamini kuwa una thamani na maamuzi yako pia yana thamani. Kujiamini huku hakumaanishi KUJIGAMBA mbele za watu , bali ni ile hali ya kujihisi na kujiaminisha kimoyomoyo kwa kujiambia kuwa muonekano wako, mtazamo wako, na maamuzi yako kwa kadri utakavyo basi yana thamani pia mbele ya wengine. Usiwe mtu wa kukubali tuu maneno ya watu na mtazamo wa watu juu yako. 
Hata hivyo hii haimaanishi kuwa usiwe msikilizaji wa maelekezo na mafunzo au kukosolewa. Pima unachokoselewa, jifunze ili ujiboreshe sio tuu usikilize kukosolewa na kujiona mnyonge.
Soma makala hizi kujua zaidi jinsi ya kuwa na uwezo wa kujiamini:

1. Umuhimu wa kujiamini wewe wewe mwenyewe. BOFYA HAPA
2. Fahamu kwa undani kuhusu kujiamini (Self Esteem) . BOFYA HAPA
Share:

0 comments:

Post a Comment