MATUMIZI SAHIHI YA “OF COURSE”, “SURE”, “SIMPLY”, “EXACTLY” NA “JUST”

Kufahamu English kwa usahihi kunakutaka ujue matumizi sahihi ya maneno kwa mazingira sahihi kwani wakati mwingine neno moja linaweza tumika. Leo tuangalia maneno ambayo mara mika katika mazungumzo , ili nawe ujue jinsi ya kuyatumia.
                  
Neno la kiingereza SURE:
Neno hili lina maana tofauti kutegemeana na matumizi. Mfano; Linaweza kumaanisha hali ya uhakika. Mfano: I am sure, it was him- Nina uhakika alikuwa yeye.                        
Wakati mwingine neno Sure linaweza kumaanisha kukubaliana na jambo. Mfano:  Unamuambia mtu “Will you teach us today ?”. Huyo mtu anaweza kukujibu "Sure". Akimaanisha kuwa bila wasiwasi atafanya hivyo.                      
Sure pia inaweza kutumika kuitikia mtu akisema ahsante, ambapo hapo itakua na maana ya 'Hakuna tatizo, au usijali" . Mfano: Thank you teacher . Mie nikajibu :" Sure".
Wakati mwingine sure hutumika kumaanisha ndio , au  hicho ndicho kilichotegemewa au kwa Kiswahili cha mtaani ni “umegusa mahala pake”. Mfano:  “Would you like tea “? Je ungependelea chai ?  Jibu: “ Sure”                        
Neno la kiingereza EXACTLY:
Neno hili lina maana ya SAWA SAWA. Neno hili linaweza pia kutumika kama jibu kuonyesha kukubaliana na alichosema mtu mwingine.  Mfano rafiki yako anasema: “We like English”. Wewe unaweza sema: "Exactly".                        

Neno la kiingereza SIMPLY:   
Neno hili lina maana ya " BILA MANENO MENGI, au KWA URAHISI " Mara nyingi hutumika kusisitiza jambo. Mfano: He is simply the best -  Bila maneno mengi jamaa yupo vizuri sana.

Neno la kiingereza JUST:
Neno hili lina maana tofauti tofauti. Maana yake ya kwanza ni kuelezea tukio limetokea muda si mrefu uliopita. Mfano: I have just arrived .(Nimewasili muda si mrefu).
Maana nyingine ya just ni kusema “sawa sawa” au “haswa”. Mfano: That is just what I need - Hicho ndicho ambacho haswa nakihitaji.
Maana nyingine ya just ni “tuu”, mfano:  I am just asking - Ninauliza tuu.
Just pia hutumika kueleza “sawa sawa” au “Kwa ukamilifu” mfano: Put your head just here - Weka kichwa chako hapa kwa ukamilifu.                      

Neno la kiingereza OF COURSE:
Tumia OF COURSE kuelezea jambo ambalo unadhani ni la kawaida tuu,  wakati mwingine humaanisha BILA SHAKA. Hata hivyo tumia of course kwa umakini kwani inabidi uhakikishe huyo unayemuambi of course anafahamu hicho unachomuambia , vinginevyo itachukulia kama dharau.Mfano: Teacher can I ask a question ? Nakakujibu: " Of course yes"

Share:

2 comments: