MAMBO 6 YA KUFANYA ILI UWEZE ENGLISH VIZURI KAMA UPO KAZINI

matumizi_ya_English_ofisini
Kama upo kazini ila kiwango chako cha English hakilidhishi ni wakati sasa umefika wa kubadili hali hiyo. Katika ulimwengu huu wa ushindani wa ajira, mabadiliko ya teknolojia na utandawazi, kujua English sio tuu kutafungua fursa, bali pia kutaimarisha nafasi yako kazini maana utakua na kitu cha ziada na utaweza kujiendeleza wewe kama wewe.

Mbuke Times chini ya mpango maalum wa Mbuke Academy tumedhamiria kukusaidia uweze kutimiza ndoto yako ya kutoka katika hiyo hali ya kutoweza vizuri English, na uwe kweli mwenye kujua vizuri English. Lengo la makala hii ni kukuelezea mambo ya kuzingatia ili uanze kweli kweli kubadilisha hali hiyo maana wengi hawajui unaanzaje anzaje ufikie kujua English kwa ufasaha.

Kuishinda aibu ya kujifunza  kuongea na kuandika English:
Wataalamu wanasema kinachohitajika sana katika kujifunza lugha ni uwezo wa kushinda uoga wa kukosea. Watu wengi hukwama kujifunza haswa wakiwa katika nafasi kama yako, wamepata elimu fulani, wana nafasi fulani ya kazi inakua ngumu kuonekana wanakosea, kwani kinachokuwa kichwani ni kuwa wao hutakiwa kuwa sahihi wakati wote.
Hata hivyo si kweli. Hakuna muda wa kuweza English, wakati wowote ukitaka kujifunza unaweza jifunza. Ishinde aibu, jipe moyo kuwa hata ukikosea , ni kukosea kwa muda tuu ila unachojitengenezea ni kikubwa kabisa.

Tambua matatizo yako yapo wapi:
Huwezi tatua tatizo kama hujui tatizo au hukubali kuwa ni tatizo. Kama wewe mwenyewe unaona sawa hicho kiwango chako cha English, haitowezekana kurekebisha na kuboresha. Achana na misemo “Kibongo bongo ndio hivyo tunaenda tuu” , au kuwa “Umri umeenda siwezi jifunza kitu tena”, au “ Cheti cha elimu ulichonacho kitanilinda ingawa sijui vizuri English”, au “Mbona wapo wengi tuu walio kama mimi”.
Kumbuka maisha yanaenda yakibadilika, fursa ulizozipata hapo mwanzo sio kama zitakazokuwepo hapo baadae, hali ya uchumi inabadilika, na hata mahitaji yako yanabadilika. English kuiweza vema inahitaji muda, usije subiri mpaka siku uhitaji kweli English fasaha , halafu ndio uanze kujifunza. Utakua ushachelewa.

Tafuta kishawishi na hamasa ya kujua English kwa ufasaha:
Bila shaka ukiwa kazini mambo mengi yanakuhitaji wewe hivyo muda wako binafsi wa kujifunza mambo ya ziada kama English huwa mdogo au “haupatikani” kabisa. Hata hivyo kumbuka msemo “ I don’t have time ; No, You Just Don’t Have Priorities”.  Hivyo mara nyingi waweza sema huna muda wa kujifunza English kwa ufasaha lakini ukweli ni kuwa kujua vema English kwako sio kipaumbele. Na njia nzuri ya kufanya kujua English kuwa ni kipaumbele chako ni kuhakikisha unatafuta sababu ya kukuhamasisha kujua English vizuri. Mojawapo ya sababu ya kukuhamasisha kujua English vizuri yaweza kuwa:
*Kutaka kufanya masomo ya juu zaidi nje ya nchi ambayo lugha kuu ya mawasiliano ni English,
*Kutaka kujua  English vizuri ili uweze kupanda cheo maana kadri unavyopanda vyeo ndivyo utakavyohitajika kuzungumza katika mikutano mbalimbali ,
*Kukutana na wageni wa kimataifa wasiojua Kiswahili, na pengine kuenda nchi ya nchi kwa mikutano, au warsha.
*Kujua English ili kuweza kuwasaidia watoto wako wanaokua na kujifunza English kwa haraka hivyo usiabike pale mtoto atakapohitaji msaada wa homework halafu mzazi huwezi vizuri au kumsaidia zoezi halafu mtoto akose kwakua ulimpa majibu yasiyo sahihi.
*Kuwa katika kiwango kimoja na rafiki zako ambao huonekana kujua English vizuri na kujieleza kwa ufasaha

Weka malengo kamili yenye muda maalum:
Haitoshi kushawishika na kuwa na hamasa ya kujua English kwa ufasaha. Hatua inayofuata ni kuweka malengo ya hatua kwa hatua kwa jinsi gani utakavyokua ukiboresha English yako. Malengo haya na mikakati yanategemea kiwango gani cha English ulicho nacho kwa sasa na rasilimali utakazoweza kupata.


Parts of speech ni muhimu sana:

Parts of speech ni mkusanyiko wa aina za maneno ambapo tunapata makundi nane tofauti kama vile nouns, pronouns, adjectives, adverbs, verbs, interjections, conjuctions na prepositions. Bila kujua vizuri hizi aina za maneno na kanuni zinazoitambulisha waweza jikuta ukiendelea kufanya makosa madogo madogo ambayo hupoteza maana inayokusudiwa. Mfano kwakua unashindwa kutofautisha na kutambua mbinu za kujua nouns, adverbs na adjectives waweza kujikuta ukichanganya matumizi ya maneno safe, safety na safely. Mfano si ajabu ukasema : I arrived home SAFE (Ukimaanisha nimefika salama nyumbani). Hapo SAFE ni adjective , haikupaswa kutumika hapo, badala yake ulipaswa kutumia adverb kwakua unataka kufafanua kuhusu tukio la kufika, hivyo ungesema I arrived home safely.

Mfano mwingine mara nyingi utaona watu wakichanganya matumizi ya YOUR na YOU’RE wakati kumbe ukifahamu vizuri aina za maneno utajisuta wewe mwenyewe kwanini ukosee kiasi hicho . Your (yaani YAKO) ni adjective, wakati YOU’RE (Wewe ni..)  ni kifupi cha  pronoun ( You) na verb ARE. Hivyo ni kosa kusema kwa mfano: Your my friend - Ukimaanisha wewe ni rafiki yangu, kwani maana yake kwa kutumia neno YOUR ni “ WAKO RAFIKI YANGU”. Hapo ungesema “ You are my friend” au “ You’re my friend” ndio sahihi.

Grammar ya kiingereza :
Grammar ni muundo mzima wa lugha ya kiingereza ikizingatia namna ya kuunda sentensi na pia namna ya kutengeneza maana iliyokusudiwa. Mfano haitoshi tuu kujua aina za maneno, inabidi ujue jinsi ya kuunganisha hizo aina za maneno ili sentensi zilete maana.
Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unajua miundo mizima ya sentensi ikijumisha nyakati (tenses), aina za maneno (parts of speech), na mambo mengine kama vile idioms, types of sentenses, phrases n.k.
Mfano sentensi hii : Iam in meeting since 6:30  this morning. Ambapo msemaji anakusudia kusema : “ Nipo kwenye mkutano tangu saa 6:30 asubuhi ya leo” Ina makosa ya kigrammar kwakua haijazingatia mambo yafuatayo:
Tense sahihi haijatumika:  Msemaji anazungumzia tukio ambalo lilianza wakati fulani na bado linaendelea. Tense inayotaja matukio  au hali ya namna hiyo inaitwa present perfect continuous tense ila msemaji ametumia Simple Present Tense. Hivyo badala ya I am … ingekuwa I have been
Article imeachwa: Kwakua msemaji anatambulisha mkutano kwa mara ya kwanza alitakiwa atumie A kama article inayoendana na  meeting, hivyo ingekua I have been in a meeting …

Hitimisho:
Inawezekana kabisa kuweza English kwa ufasaha. Inahitaji makusudio ya dhati toka kwako kuhusu kujifunza English, na upate msaada wa karibu wa mtu atakayekusaidia. Tuwasiliane kwa namba +57 301 297 1724 WhatsApp au kwa email john.myungire@gmail.com ili nikusaidie kupanga mkakati na hatimaye ujifunze kwa mafanikio.
Nimeandika kitabu pia cha English chenye maelekezo ya kutosha kuhusu Grammar. Kitabu kinapatikana pia tuwasiliane.
Share:

0 comments:

Post a Comment