WhatsApp ina faida nyingi ukiachilia mbali kuwezesha marafiki na ndugu na jamaa kuwasiliana. Faida nyingine ni kuwa WhatsApp inaweza kutumika kuunganisha asasi/biashara na walengwa wake, au watu kutengeneza makundi ya kujifunza na kupashana habari mbalimbali.
Hata hivyo usipojua kuitumia vizuri WhatsApp inaweza kuwa kero. Kwa mfano kuna meseji za zamani unataka kuzisoma ila haujui utafanyaje uzisome maana ni nyingi inabidi uchambue meseji nyingi mpaka ufikie meseji unayotaka.
Makala hii inakupa mbinu mbalimbali ili uboreshe matumizi yako ya WhatsApp:
Kusearch katika WhatsApp
Badala ya kutafuta meseji au neno fulani kwa muda mrefu unaweza kutumia huduma ya Search. Angalia picha zifuatazo ili ujue jinsi ya kusaearch.
Bofya hicho kialama cha SEARCH angalia mshale hapo juu. Kisha andika neno au sentensi unayotaka kuisearch |
Mfano wa jinsi ya kusearch, ukiandika neno kisha ukabofya enter , utaletewa meseji tofauti tofauti kuendana na wapi haswa unachosearch kimo. Click meseji unayotaka kusoma kisha endelea kusoma. |
Kujibu Meseji Husika Tuu
Kuna wakati inakubidi badala ya kutoa tuu jibu inabidi umuonyeshe unayechat nae kuwa jibu unalotoa ni kwa ajili ya meseji fulani husika.
Angalia picha zifuatazo:
Huu ni mfano wa jinsi ya kuunganisha meseji unayotaka kujibu ili msomaji ajue jibu lako linahusu haswa meseji gani.
Ili ufanikishe kuunganisha meseji yako na meseji ya mtu mwingine fanya ifuatavyo:
|
Ukibofya kimshare katika kimshare namba 2 katika picha iliyotangulia utaletwa kwenye sehemu ambapo meseji husika itakua imeunganishwa na wewe utaweza ona sehemu ya kuandika meseji yako. Andika meseji yako kisha itume, mpokeaji ataona meseji uliyotuma na ile ambayo umeiunganisha.
Nice
ReplyDeleteElimu Yesu ni nzuri
ReplyDeleteIp pw sana
ReplyDelete