UNATAFUTA KAZI ? MBINU HII ITAKUSAIDIA


Nikupe changamoto leo wewe unayetafuta ajira. Kabla haujatuma maombi ya kazi jiulize wewe kama wewe unaweza kuifanyia nini kampuni au asasi husika ? Je una ujuzi gani haswa au ni mambo gani haswa unaweza kuyafanya ambayo yatakua ya muhimu katika hiyo kampuni au asasi unayofikiria kuomba nafasi ya kazi ?
Kumbuka muajiri haajiri CHETI chako, haajiri CHUO ulichosoma. Anachohitaji haswa NI WEWE KAMA WEWE na hali yako ya kujituma, kufikiria , na utayari wako wa kuingiza kitu katika asasi husika. 
Jipime mwenyewe kwa kuanza hivi: Nenda kwa website ya asasi au kampuni husika, kama hawana website basi omba vipeperushi au maandishi yoyote yanayoelezea kampuni au asasi husika. Soma kuhusu shughuli zao, bidhaa zao, muundo wao wa uongozi, malengo yao, changamoto zao n.k.
Kisha jilinganishe wewe kwa ujuzi wako , nini unaweza kufanya ktk uzalishaji wa hiyo asasi, nini unaweza ongezea katika usimamizi, jiulize wewe kama ndio ungekuwa mfano meneja wa masoko ungefanya vitu gani tofauti, au wewe ndio ungekuwa computer programmer wa hiyo asasi au kampuni ungetengenezaje website au apps zenye kuiboresha hiyo asasi n.k
La msingi ni kuwa kabla haujaomba kazi katika asasi au kampuni husika jiweke ndani ya hiyo asasi au kampuni halafu jione kwa kiwango gani una fiti na kuwa wa muhimu. 
Kama ukijipima wewe mwenyewe na kujiona haufikii basi jiulize wapi ktk ujuzi wako, wapi ktk sifa nyingine unahitaji kuongeza.
Share:

0 comments:

Post a Comment