Picha za Ronaldo toka Mirror.co.uk |
TUJIFUNZE KITU HAPA..
Tuache ushabiki wa Messi na Ronaldo. Kuna habari nzuri nataka kushare nawe.
Bila shaka unapenda mafanikio lakini je una MOYO wa MTU WA MAFANIKIO ? Je unajiona wa kufanikiwa ? Je unajitoa mpaka mwisho au una ahirisha ahirisha mambo ukijiambia kuwa bado una muda. Au pengine unajiambia huwezi ?
Fikiria hizi picha za Ronaldo, yaani hapo yupo nje tuu ya uwanja hali yake ni hivyo, je akiwa uwanjani huwa anacheza kwa kujituma kiasi gani ? Ushindi bila shaka hauanzi tuu katika kufanya jambo husika, inabidi kwanza ujisikie wewe ni mshindi.
Si mara ya kwanza kumsikia Ronaldo akihojiwa na kusema alicheza kwa matumaini makubwa ya kushinda, na alijisikia kabisa kushinda. Mfano katika fainali za UEFA akiwa na Real Madrid alidai alisikia kabisa sauti ndani yake ikimuambia kuwa yeye ndiye atakayefunga penati ya ushindi.
Kwenye mashindano ya UERO 2016 yule mfungaji wa Ureno katika fainali hizo alihojiwa na kusema kuwa Ronaldo alimtia moyo sana wakati wa mapumziko na kumuambia anaamini yeye Eder angefunga goli la ushindi.
Sio hivyo tuu kwenye robo fainali , Ronaldo alimpa moyo Moutinho ambaye alionekana kujitenga ili asiende kupiga penalty. Katika video iliyosambaa mtandaoni Ronaldo anasikika akimuambia Courtinho " Njoo , unapiga vizuri penati, kuwa hodari, njoo, kuwa hodari, najua unazipiga vizuri penati". Na kweli Courtinho alifunga hiyo penati.Come. Video ya Ronaldo akimpa moyo Moutinho ipo hapa.
Nataka nikupe moyo wewe pia, jijengee mazingira na kujiamini, kuwa hodari, jione kabisa kuwa unaweza, kwani kama wewe mwenyewe ukijiambia huwezi, basi itakuwa ngumu sana kujituma na kufikia malengo unayotaka, kwani inahitaji kujitoa kwa hali ya juu, na kujitoa huko kuna wezekana endapo tuu ukiona na kuamini katika mafanikio yako. Jione mshindi, jione unaweza.
Na kama malengo yako ni kujua ENGLISH kwa ufasaha, au unaongopa kuongea English au unapata shida kuelewa mtu akiongea English, basi tuwasiliane nikupatie hiki kitabu nilichokuandika kwa maelezo mepesi kanuni muhimu za lugha ya kiingereza. Jipe moyo, unaweza.
0 comments:
Post a Comment