Kama una tatizo la kujua tenses, basi soma makala hii itakusaidia sana .
Ili uongee na kuandika kiingereza kwa usahihi unahitaji kufahamu kanuni za jinsi ya kuunganisha maneno utakayotaka kutumia. Hivyo basi kujua tuu maana ya maneno bila kujua jinsi gani utayaunganisha hakutokusaidia sana. Maneno katika lugha yameganywa katika makundi mbalimbali kama vile vitendo (verbs), nomino (nouns), viwakilishi (pronouns) n.k
Kujifunza tenses katika kiingereza ni kujiwezesha kujua kwa namna gani utaunganisha vitendo (verbs) na maneno mengine kwa usahihi. Na kwakua mara nyingi tunahitaji kuongelea kuhusu vitendo/matukio , usipofahamu matumizi sahihi ya tenses, unajikuta upo na wakati mgumu sana wa kuongea English sahihi.
Usihofu, baada ya kumaliza kusoma makala hii utakuwa na mwanga mzuri na utakuwa umeboresha ufahamu wako kuhusu tenses katika English. Hata hivyo nikutaarifu tuu kuwa makala hii ni ndefu, na nakuomba usome kwa umakini hatua kwa hatua maelezo yafuatayo ili uweze kweli kutoka na kitu katika makala hii. Note: Maelezo haya ni uchambuzi wa maelezo yaliyopo katika kitabu nilichoandika cha ENGLISH : Mbinu na Kanuni za Kuijua.
Tuwasiliane kwa WhatsApp nikupatie copy yako. +57 301 297 1724
Vitenzi (Verbs) ni nini ?
Vitenzi au kwa kiingereza verbs ni maneno ambayo yatoa taarifa kuhusu matukio au hali fulani. Mfano wa vitendo ni kama vile EAT - Kula, WRITE - Andika, SLEEP- Lala maneno ambayo yanaelezea matukio. Halaf mfano wa maneno yanayoelezea hali ni kama vile IS -ni, ARE-ni, WERE - kuwa (wakati uliopita), WAS -kuwa (wakati uliopita), WILL BE.
Vitenzi pia hutumika kutaja umiliki , kama vile HAS, HAVE, WILL HAVE, n.k
Uhusiano kati ya verbs na tenses
Matukio , kumiliki au hali fulani hutokea katika nyakati tofauti, hivyo basi ili tufikishe ujumbe sahihi na uliokusudiwa inatupasa tuelezea matukio, hali au kumiliki kwa wakati sahihi. Mfano sentensi zifuatazo hazieleweki kwa haraka kwakua tumechanganya nyakati husika:
John aliimba muziki kesho.
Yeye anakula chakula jana.
Agness alikuwa mama wiki ijayo.
Unajua tense sahihi ya kutumia ?
Ili uweze kutumia tense sahihi inakubidi ujue utofauti wa nyakati (tense) na hali ya tense(situation). Hapa ndipo penye utamu wa tenses, na ni rahisi sana, kwani kwa ujumla wake tuna tenses TATU tuu, yaani PAST, PRESENT na FUTURE.
Halafu tuna hali NNE tuu, yaani Continous, Simple, Perfect , na Perfect Continous.
Hapo kumbuka kuwa hali zimo ndani ya tenses, hivyo basi kwa kila tense , utapata hizo hali nne, kwa maana ya kuwa tuna:
Past Continous
Present Continous
Future Continous
Past Simple
Present Simple
Future Simple
Past Perfect
Present Perfect
Future Perfect
Past Perfect Continous
Present Perfect Continous
Future Perfect Continous
Urahisi wa kujifunza tenses upo hapa
Unaweza jifunza tenses kwa kuangalia vitu vinavyojitokeza kwa ujumla kwa makundi fulani ya hali za tenses. Soma kwa makini muongozo ufuatao:
Hali ya continous : Tunatumia hali hii kuelezea tukio linalofanyika kwa wakati husika. Mfano :
Present continous : I am writting this article Yaani wakati huu huu ninaandika.
Past continous = I was writting this article. Yaani nilikuwa nikiandika makala hii.
Future continous : I will be writting this article Yaani nitakuwa nikiandika makala hii.
Utagundua kuwa tunatumia continous kuelezea tukio ambalo halijamalizika kufanyika, linaendelea kutendwa.
Kingine cha kugundua ni kuwa haijalishi ni wakati uliopita , ujao au uliopo, ili mradi ni CONTINOUS , basi verbs za matukio lazima ziishie na ING. Kuishia na ING maana yake ni kama vile writtING, openING, watchING.
Hali ya perfect : Tunatumia hali hii kuelezea tukio ambalo tayari limekwishamalizika kufanyika. Mfano:
We have eaten - Tumekwisha kula.
We had eaten - Tulikua tumekwisha kula.
We will have eaten. - Tutakua tumekwisha kula
Utagundua kuwa haijalishi iwe ni past, present au future, ili mradi tuu tukio limekamilika unatakiwa kutumia hali ya perfect.
Pia utagundua kuwa kwa perfect zote , verbs zinatakiwa ziwe katika hali inayoitwa past participle. Mfano : go (kuenda) inakua - gone, write - written, cook - cooked, n.k. Kujua past participle ya verbs inabidi ufanye mazoezi maana zipo verbs nyingi sana na zinatofautiana namna ya kuziweka katika past participle.
Badala ya kuelezea hali ya simple, ngoja kwanza nikufafanulie mambo mengine ya msingi ya kuangalia ili uwe na matumizi sahihi ya tenses :
Kuna kitu kinaitwa Auxiliar verb:
Mara nyingi ili kutambulisha tupo katika tense na hali fulani, huwa tunahitaji vitu viwili, kwanza kuweka VERBS za matendo katika hali sahihi, mfano kama ni hali ya continous tumekwisha ona hapo juu tunatumia ING, kama go inakuwa going, halafu kama ni ya perfect basi verbs lazima ziwe katika past participle mfano eat - eaten.
Hata hivyo tumeona kuwa kabla ya verbs kuna maneno mengine yanatumika kutambulisha tupo wakati gani.
Mfano :
He is going to school - Anaenda shule
He was going to school. - Alikua akienda shule
He will be going to school. - Atakua akienda shule
Angalia sentensi hizo hapo juu, tunaelewa zote ni continous kwakua verbs za tukio zinaishia na ING. Hata hivyo, ingekuwa ngumu kujua ni Continous ya wakati uliopita , ujao au uliopo endapo tusingekuwa na maneno IS, WAS, na WILL BE.
Hayo maneno yanayoongezewa ili kurahisisha kutambua tupo wakati gani , huitwa auxiliary verbs.
Kwanini lazima ujue auxiliary verbs kwa kila TENSE:
Kutambulisha wakati husika:
Kama nilivyotoka kueleza hapo juu, kama tusingekua na auxiliary verbs tusingejua tunazungumzia wakati gani. Namaanisha hivi:
He going to school.
He going to school.
He going to school.
Hizo sentensi tatu zinaonekana kufanana na wala hazituelezi tupo wakati gani, tunachojua tuu ni kuwa kitendo kinaendelea. Hivyo kuweka IS, WAS, na WILL BE hapo kabla ya verb going, kunatusaidia kujua tupo wakati gani.
Kukanusha sentensi
Ili kukanusha sentensi inabidi kutambua auxiliary verb husika inayoenda na personal pronoun au noun husika. Mfano :
We are not eating now. Hatuli wakati huu. Hapo tumeona mbele ya auxiliary verb tumeweka not. Tungeweza kuandika We’re not eating now.
They have not gone. Wao hawajaondoka . Tumeona pia mbele ya auxiliary verb have, tumeweka not. Tungeweza andika They’ve not gone.
Kuuliza maswali
Ili kuuliza maswali inabidi kutambua auxiliary verb husika inayoendana na personal pronoun au noun husika, kisha anza na hiyo auxiliary verb katika swali husika.
Mfano
Are we going to school ? - Je tunaenda shule ?
Have you eaten ? Je umekula ?
Unazijuaje auxiliary verbs za kila tense ?
Kama tulivyoona hatuna tenses nyingi na hali nyingi, hivyo basi tafuta muda usome kuhusu verbs na muunganiko wake na tenses, na fanyia mazoezi mara kwa mara mpaka zikukae kichwani.
Kitabu cha MBINU ZA KUIJUA ENGLISH nilichoandika ambacho kinapatikana kwa Tshs. Elfu Kumi na Tano , kina maelezo mazuri sana kuhusu auxiliary verbs, personal pronouns na tenses kwa ujumla. Wasiliana nami kwa WhatsApp kwa namba hii ujipatie makala yako :+57 301 297 1724
Au nicheki kwa Facebook kwa www.facebook.com/mbuketimes
well good i learn something
ReplyDeleteit's wonderful i really like the subject..
ReplyDeleteGood
ReplyDeleteNaomba unitumie copy WhatsApp pdf tafadhal my no 0679183540
ReplyDeleteNaomba unitumie copy WhatsApp pdf tafadhal my no ni 0679183540
ReplyDelete