Kama haukujua basi jua kuwa:-
Mtandaoni humu kuna habari nyingi ambazo zinaweza kuonekana ni kweli ila ni za uongo. Na watu wengi wameingizwa "mkenge" kwa kunukuu habari za zisizo na ukweli (bandia) wakidhani ni za kweli. Tambua kuwa kuna websites zimeandaliwa maalum kwa ajili ya kukebehi na kuchekesha kwa kutumia habari zenye kusomeka kama kweli ila ni uzushi tuu. Kwa kiingereza habari hizo huitwa Satire News.
Unakumbuka habari hizi ?
1. Bingwa wa zamani wa ngumi za kulipwa Mike Tyson abadili jinsia yake. Bofya hapa
2. Mugabe asema Mandela alikuwa muoga, na anayestahili kupewa sifa ni yeye Mugabe. Bofya hapa
3. Watu 37 wafariki dunia kwa kuvuta bangi baada ya kuzidiwa kwa kuwa sasa bangi imeruhusiwa Marekani. Bofya hapa
4. Obama kufadhili msikiti kwa fedha zake huko Marekani ? Bofya hapa
5. Picha ya uongo ya mwigizaji Paul Walker alipopata ajali iliyopelekea kifo chake. Bofya hapa
Jitahidi unaposoma habari ufanye utafiti zaidi hususani kama unataka kuiweka habari hiyo kwa chombo chako cha habari iwe blog, website , TV au kuirusha redioni.
Ifuatayo ni orodha ya websites zinazojulikana sana kwa habari feki au bandia:
1. NewsBiscuit.
3. The Onion
4. Private Eye
5. The Spoof
7. Fake a Wish
10. The Gatsby
0 comments:
Post a Comment