Ili kukuletea habari unazoona katika ukurasa wako wa habari ( unaitwa News Feed) , kampuni ya Facebook inatumia utaratibu maalum wa kuweza kufanya hivyo. Utaratibu huo unaitwa Algorithm.
Mara kwa mara kampuni hiyo hufanya mabadiliko katika algorithm yake kuendana na malengo waliyojiwekea.
Hivi karibuni Facebook imebadili namna algorithm yake inavyofafanua aina gani ya posts uzione katika feeds.
Kwa kiwango kikubwa imekusudia kutokuzipata nafasi picha za vichekesho tuu, na kuweka msisitizo kwenye habari muhimu kwa ajili yako. Hayo ni kwa mujibu wa makala hii toka Facebook.
Facebook wanachoangalia kikubwa ni kwa namna gani post imepata kuwa shared au kupata Likes nyingi ndio basi hiyo ndio itakayopewa nafasi.
Hivyo kama posts zako hazina likes au comments nyingi basi waweza kuta isiende kwa watu wengi.
Hata hivyo kama hiyo haitoshi, kuna habari nyingine unapaswa kujua kuhusu nani ataona posts zako:
Kwa mujibu wa EDGE RANK - yaani hiyo algorithm ya FB, ni kuwa wanaoona posts zako ni wale ambao kweli upo nao karibu nao kimawasiliano. Hivyo haijalishi ni friends wangapi unao, bali wale ulio nao karibu - yaani unao comment posts zao, kulike posts zao, na wale wanaofanya hivyo kwako hao ndio ambao watakuwa na nafasi ya kwanza kuona posts zako.
Tena kwa mpango mpya wa Facebook ni kuwa hao ulio nao "karibu" kimahusiano FB ndio pia wataweza kuona posts hizo na kupewa updates hata kama siku zimepita toka post husika iwe hewani. Ni kwamba wanapewa muendelezo wa stori ilivyokuwa.
Ndio maana ushishangae hivi sasa unaweza kuona stori ya zamani kidogo kwa news feed yako ukasema inakuaje FB wanaweka kitu cha zamani, angalia vizuri utagundua inazungumzia comment ya siku hiyohiyo ingawaje post ni ya zamani.
La ziada, ni kuwa FB ili kukusaidia kupata habari muhimu, kama ukibofya link ya post fulani katika news feed yako, basi utaletea mapendekezo ya habari nyingine ambazo pengine zitakuvutia kusoma.
0 comments:
Post a Comment