MAREKANI ULIYOIFAHAMU SIO YA SASA: FAHAMU MATUKIO HAYA YA AJABU MITAANI

KAMA HAUKUJUA BASI JUA
Nchini Marekani hususani kwa jiji la New York, Philadelphia, Chicago, St Louis na San Diego kumezuka tabia ya vijana kushambulia watu mtaani , hata hivyo sio kuwashambulia kwa maana ya uporaji, bali ni kuwavizia watu kisha kuwapa kipigo kimoja cha nguvu -mara nyingi kipigo humfanya mtu aanguke chini.
Vijana hao hufanya hivyo kama sehemu ya mchezo "Game" ambayo imepewa jina la KNOCK OUT GAME.
Lengo haswa la kufanya hivyo? 
Ni kama burudani tuu kwao, na wengine hurekodi matukio hayo na kuyarusha YouTube.
Hivyo watu mitaani wamekuwa wakitembea kwa wasiwasi kwani yawezekana bila kujijua ukashangaa umepiga bonge la ngumi au kofi , mpaka unaanguka, kisha mtu huyo aliyekupiga anakimbia zake.
Matukio haya yameripotiwa na vyombo vya habari mbalimbali kama telegraph.co.uk, dailymaily.co.uk na CNN. 
Katika tukio la ijumaa iliyopita Jan.17 2014, DailyMail.co.uk inaripoti kuwa mtu mzima mwenye umri wa miaka 74 alishambuliwa na vijana huko Dallas.
Cheki video  hii ikielezea matukio hayo ya Knock Out Game:

Share:

0 comments:

Post a Comment