Unakosea unapojiwekea kikomo cha aina gani ya mtu unayeweza kuwa. Kumbuka unaweza kuwa bora zaidi ya hapo unapodhani umefika. Ngoja nikupe mfano:
Ulipozaliwa -haukuwa mwalimu, nesi, au mhasibu.
Uliingia shule ya msingi -ukasoma yale yaliyokuwepo kama watoto wengine wa kitanzania.
Ulipoingia sekondari pengine ndio mambo yakabadilika. Kwa sababu pengine zilizo nje ya uwezo wako ukasoma mambo ya biashara, au ya sayansi, au sanaa (arts). Nasema sababu zilizo nje ya uwezo wako kwakuwa pengine ulifuata mkumbo, pengine wazazi ndio walitaka usome hivyo, pengine shule uliyosoma ilikufanya usome yale uliyosoma.
Pengine umebahatika kwenda hadi chuo ukasoma uliyosoma.
Si unaona hayo yote ni matokeo tuu ya mazingira uliyokumbana nayo -hayajabadilisha uwezo wako kama mwanadamu wa kujifunza. Kama uliweza jifunza kitu fulani , waweza pia kujifunza kitu kingine ukiweka nia. Ila bahati mbaya SIVYO unavyoamini.
Umejiaminisha kuwa kwakuwa wewe ni MHASIBU, basi hautoweza kujifunza teknolojia. Umejiamini kuwa kwakuwa wewe ni mtu wa ARTS basi ingawa unapenda uhasibu hautoweza kusoma kwakuwa wewe "si mtu wa mahesabu".
--Pasipokuwa na nia hata njia haitoonekana, ila palipo na NIA pana njia. Usikubali kufanya kazi usipoyoipenda, isiyokulipa na kuendelea kulalamika kuwa hauna mafanikio wakati kuna njia nyingine za kuwa bora zaidi. UNAWEZA kuwa hivyo unavyohisi moyoni ungependa kuwa. Ondoa vizuizi vya kifikra ulivyojiwekea.
Nikuache na msemo huu toka kwa raisi Baraka Obama:
"Change will not come if we wait for some other person or some other time. We are the ones we've been waiting for. We are the change that we seek."
"Mabadiliko hayatokuja kama tukimsubiri mtu mwingine afanye mabadiliko au tusubirie wakati mwingine. Sisi ndio ambao tumekuwa tukisubiri mabadiliko. Sisi ndio mabadiliko tunayotaka kuwa."
0 comments:
Post a Comment