TAFAKARI YA LEO

Fans jumanne njema.
Tafakari yetu leo ni:

Kwamba kama kuna giza haisaidii kuwa na gropu isiyowaka, au taa nyingine kama ya chemli isiyowaka huku ukisema unataka kuleta mwanga.
Kinacholeta mwanga lazima kwanza kiwashwe, lazima kwanza kitoe mng'ao ili kisaidie.
Tuna matatizo mengi katika jamii, familia zetu na hata sisi wenyewe binafsi. Fananisha matatizo hayo na GIZA, na kwamba wewe una mchango mkubwa katika kuyatatua. 
Ila kama wewe mwenyewe haujang'aa, kama wewe mwenyewe haujajiweka kutoa mwanga, giza halitoondoka.
Kumbuka kuwa na fedha , cheo au mali fulani ni lengo yaani ni kitu cha mwisho na sio mchakato. Mchakato ni wewe kujiboresha kiujuzi iwe teknolojia, uongozi, kilimo n.k, jiboreshe kiufahamu wa mambo ya msingi kama mawasiliano, kujitambua, mahusiano, jenga mtandao wa kukusaidia, na jijengee mtazamo chanya wa maisha kwa kuamini unaweza kufanya makubwa. Hata kama unadhani leo hii umefanikiwa. Bado waweza fanya bora zaidi ya hapo.
Share:

0 comments:

Post a Comment