Poke: Neno
hili linamaanisha kuwa ni kutoa salamu ya juu juu kwa mtu husika ambaye
unampoke. Na pia kinachotokea ni kuwa kama huyo mtu atakupoke pia kurudishia
poke yako ni kwamba hata kama sio mmoja wa Friends wako, basi unakuwa umemruhusu awe na uwezo wa
kucheki wasifu wako (profile) yako. Kwani mara nyingi kama mtu sio rafiki yako,
na ume iset profile yako watu wasione
profile yako hawawezi kuiona, ila kwa kujibu poke ya mtu asiye rafiki yako, unampa nafasi
ya kuona profile yako, na wewe pia waweza ona profile yake.
Fans: Kama una ukurasa maalum wa FB, tunaita
Facebook Page, basi wale ambao wame LIKE ukurasa huo ni fans wako. Yaani
washabiki au watu wenye kuupenda huo ukurasa.
Friends: Kama una akaunti yako binafsi basi wale ambao
wanatajwa kwenye wasifu wako kama Friends hao ndio waweza kuwaita friends. Kitendo cha kuongeza friends wako wa FB
tunasema una ADD friends.
Members: Kuna
makundi mengi katika FB unaweza kujiunga. Basi wale ulionao pamoja kwenye kundi
husika ni wana kikundi wenzako, au tunaita MEMBERS. Haipendezi kuita
waliojiunga na kundi lako kuwa ni FANS.
Tagging :
Unapomtag mtu mwingine iwe picha au status tuu ya maandishi ina maana kuwa
unataka yafuatayo yafanyike : Kwanza picha hiyo ionekane kwenye akaunti ya huyo
mtu kana kwamba huyo mtu aliweka picha hiyo. Pili unataka rafiki za huyo
unayemtag waone hiyo picha.
Hashtag: Unapotumia alama hii # ni kwamba unataka post husika ijumuishwe
kwenye kundi la posts nyingine ambazo pia zimetumia neno ambalo wewe umetumia
na hiyo #. Mfano kama umeandika status
kisha ukaweka kama hivi #specialone basi ukibofya hilo neno special one kwenye status yako utaona utaletewa mjumuiko wa posts nyingine zilizotumia hilo neno. Angalia mfano pichani hapo chini.
Follow: Juu ya
profile ya rafiki yako utaona neno Follow au Following . Utaona neno Follow kama haujachagua ku follow,
na kama umechagua basi utaona inaonyesha Following. Maana ya neno hilo ni kuwa
unachagua kufuatilia posts zake huyo mtu kwani inawezekana mtu akawa rafiki
yake ila usiamue kufollow hivyo hautoona posts zake.
Subscribe: Mara nyingi utaona neno hili juu ya profile ya
mtu ambaye tayari amefikisha kikomo cha idadi ya marafiki anaoweza kuwa nao FB,
au ameamua kuset hiyo button ionekane kwa profile yake.
0 comments:
Post a Comment