Bila
shaka unapata manufaa kadha wa kadha kupitia internet. Je, unaingiza fedha
kupitia mtandao, au wewe ni mtu wa kutumia tuu fedha kwa ajili ya internet
lakini bado haujaanza kuingiza fedha kupitia mtandao? Makala hii inachambua
namna ambavyo unaweza kutumia internet kuingiza kipato.
1.Kutafutia watu taarifa: Wapo watu wengi wenye shida ya kupata taarifa fulani
kwa uharaka na kwa usahihi, hata hivyo wanakumbwa na vikwazo vingi kama vile wapo
‘bize’ sana –hata kama wanayo kompyuta na internet connection masaa 24, au
pengine ni kwakuwa hawana ujuzi wa kutosha wa kupata taarifa kwa ufanisi zaidi.
Watu wa aina hii pengine ni wanafunzi wa elimu ya juu, wafanyabiashara au
watafiti wa fani mbalimbali. Uwezo wako
wa kutafuta taarifa kwa ufanisi, na kuweza pia kutambua wateja walengwa wa
huduma hii , kunaweza kukufanya kuingiza kipato.
2.Kuuza bidhaa kwa bei poa kabisa: Kupitia internet utaweza kupata taarifa za bei
za bidhaa mbalimbali. Umakini na juhudi zako za kutafuta bei nafuu zaidi
kunaweza kukufanya ukajua bei poa kabisa za bidhaa fulani, kasha ukatafuta
wateja wa kuwauzia bidhaa hizo. Jambo hili limerahisishwa sana siku hizi kwa
kutumia mitandao ya kijamii kwani wapo
watu tayari ambao huingia kwa mitandao ya kijamii kama Facebook, wakitaja aina
ya bidhaa wanazotafuta. Tembelea NIPENI DILI group la Facebook, utajiona fursa
hii.
3.Kutangaza bidhaa za watu/makampuni: Kupitia mtandao mkubwa utakaoweza kujenga kwa
kutumia internet, utaweza kutangaza bidhaa za watu au asasi mbalimbali. Mfano
waweza tangaza bidhaa za watu kupitia blogu yako(yenye wasomaji wengi), au
kupitia ukurasa wako wa Facebook, au kupitia huduma maalum ya kutangaza kwa
barua pepe, ambapo utawaomba watu wajiandikishe kupata updates mbalimbali
ikiwemo matangazo ya ofa mbalimbali za
bidhaa. Waweza pia tangaza bidhaa kwa website/blogu yako kwa kupitia
Affiliate programs, ambapo utalipwa kuendana na ‘clicks’ zitakazoingiza wateja
kwa asasi fulani.
4.Kutangaza bidhaa zako: Kuna njia nyingi za kutangaza bidhaa zako kupitia
internet, kuanzia kutangaza bure au hata kulipia matangazo yako. Waweza kutumia
akaunti yako ya Facebook au GooglePlus
kutangaza bidhaa zako. Waweza tengeneza blogu
na kupitia blogu hiyo ukaweka matangazo yako. Au ukaamua kulipia
matangazo kwa blogu za watu wengine, ukatangaza kupitia Facebook, na website
mbalimbali.
5.Kuandaa kipato kikubwa cha baadae:
Ukiachilia kupata kipato cha haraka haraka kwa wakati huu, unaweza kutumia
mtandao kuandaa mapato makubwa ya baadae. Unaweza kufanya hivi kwa kutumia
internet kujenga mtandao utakaokusaidia hapo baadae-mfano kutumia Linkedin,
Facebook au Twitter kujenga mahusiano na watu ambao baadae watakuwa wateja wa
bidhaa zako, au washirika katika biashara, au hata waajiri wako wa baadae. Pia
waweza kutumia internet kujenga ufahamu na ujuzi fulani ambao hapo baadae
utaweza tumia ujuzi huo kuingiza kipato. Mfano kuna website nyingi zinazotoa
mafunzo bure ya ujuzi adimu kama website design, programming, marketing, n.k.
Hitimisho
Ukitafakari
maelezo hapo juu , utaona kuwa kuna mianya mingi ya jinsi ya kuingiza kipato
kwa kupitia internet. La msingi ni matumizi yako ya busara ya internet, na
kuendelea kujifunza siku hadi siku namna bora ya kuboresha matumizi yako ya
internet. Hata kama kwa sasa unadhani unaingiza kipato cha kutosha,
hautodhurika kwa kujifunza njia nyingine za kuongeza kipato chako.
Sawa bana
ReplyDeleteOcky
ReplyDelete